loader
Dstv Habarileo  Mobile
Picha

YANGA, AZAM VITA NAFASI YA PILI

YANGA jana ilishindwa kulipa kisasi na kulazimisha suluhu dhidi ya Azam FC katika mchezo wa Ligi Kuu Tanzania Bara uliochezwa Uwanja wa Taifa Dar es Salaam.

Kwa matokeo hayo, bado Simba inaendelea kuongoza ligi ikiwa na pointi 75 na Azam FC wanaendelea kushika nafasi ya pili ikiwa na pointi 58 zikitofautiana na pointi mbili na Yanga ambao wanasalia kwenye nafasi ya tatu ikiwa na pointi 56 na zote zimecheza michezo 30.

Hiyo ni sare ya pili mfululizo kwa timu ya Yanga katika michezo mitatu iliyocheza tangu Ligi Kuu Tanzania Bara irejee tena baada ya janga la corona ambapo mechi iliyopita ilitoka sare ya bao 1-1 na JKT Tanzania mchezo uliofanyika Uwanja wa Jamhuri Dodoma.

Katika mchezo wa awali, Yanga iliifunga Mwadui FC kwa bao 1-0 wakati wapinzani wao Azam wamecheza michezo miwili na kushinda mmoja dhidi ya Mbao kwa mabao 2-0.

Mchezo wa jana ulianza kwa kasi kila mmoja akipania kupata ushindi ili kuongeza idadi ya pointi na Azam walionekana kutawala mchezo ambapo wachezaji Never Tigere, Mudathir Yahya na Brayson Raphael walionana vyema, huku Yanga wakijaribu kufanya mashambulizi ya kushtukiza kwa kumtumia Jafar Mohamed na Deus Kaseke.

Kila timu ilitengeneza nafasi ambazo walishindwa kuzitumia na hadi zinakwenda mapumziko, hakuna timu iliyofanikiwa kupata bao.

Kipindi cha pili kila timu ilifanya mabadiliko ambapo kila upande ulionekana ulicheza soka la kuvutia hadi mwamuzi Elly Sasii ambaye alisaidiwa na na Soud Lila na Mbaraka Haule wote Dar es Salaam anapuliza kipyenga cha kumaliza pambano hilo, hakuna timu iliyofanikiwa kufamania nyavu za mpinzani wake.

Baada ya mchezo huo, Yanga itasubiri tena mpaka Juni 24, ili kuikabili Namungo FC kwenye mtanange utakaopigwa Uwanja wa Taifa, wakati Azam watasafiri kuelekea Bukoba kuivaa Kagera Sugar kwenye Uwanja wa Kaitaba.

Kikosi cha Yanga kilikuwa: Metacha Mnata, Deus Kaseke, Jaffar Mohamed, Kelvin Yondan, Said Juma ‘Makapu’, Feisal Salum , Haruna Niyonzima, Mapinduzi Balama/Mrisho Ngassa (dk 64), Ditram Nchimbi/Abdulaziz Makame (dk 79), Patrick Sibomana/Bernard Morrison (dk 46) na David Molinga/Yikpe Gislain (dk 64).

Azam FC: Benedict Haule, Nico Wadada, Salmin Hoza, Abdallah Kheri, Oscar Masai, Mudathir Yahya, Iddi Kipagwile/Bruce Kangwa (dk 60), Bryson Raphael, Rochard D’jodi/Andrew Simchimba (dk 69), Never Tigere/Shaaban Iddi Chilunda (dk 60) na Iddi Suleiman ‘Nado’.

MABINGWA wa Ligi Kuu Tanzania Bara, Simba wametajwa katika tetesi ...

foto
Mwandishi: Tuzo Mapunda

Post your comments

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi