loader
Dstv Habarileo  Mobile
Picha

NDEMLA, KICHUYA, MLIPILI WAMKUNA SVEN

KOCHA wa Simba, Sven Vanderbroeck amesema kama Said Ndemla, Shiza Kichuya na Yusuph Mlipili wataendelea kuonesha kiwango kizuri kwenye mazoezi hatosita kuwapa nafasi ya kuanza kwenye michezo iliyosalia Ligi Kuu Tanzania Bara.

Kwa muda mrefu wachezaji hao ambao wamewahi kuwika na kikosi hicho kwa misimu ya nyuma na kupendwa na mashabiki wa timu hiyo muda mwingi walikuwa wanasugua benchi.

Akizungumza Dar es Salaam jana, Sven alisema kikosi kilichoundwa na wachezaji hao na kuibuka na ushindi wa mabao 3-0 dhidi ya Mwadui FC katika mchezo uliochezwa Uwanja wa Taifa, kilicheza vizuri na kuongeza kuwa wachezaji hao wamebadilika na wanajua majukumu yao.

“Najua mashabiki wamekuwa na furaha baada ya kuwaona wachezaji kama Said Ndemla na beki Yusuph Mlipili na majina ya wachezaji wengi waliocheza wakicheza tena katika kiwango kikubwa.

‘Wamebadilika na wanajituma kwenye mazoezi na niliwaambia wachezaji wote kuwa atakayejituma hatosita kumpanga kwenye kikosi chake,” alisema

Pia alisema wachezaji wote walionesha ubora ulichangia kupata ushindi huo na kusisitiza utayari wa kila mchezaji ikiwemo mshikamano miongoni mwao ndiyo taswira anayotamani kuiona kwenye mbio za kutetea taji lao.

Sven alisema kwenye mchezo huo wachezaji walipambana na kupata ushindi mnono tangu kikosi hicho kimerejea kwenye michezo ya ligi baada ya janga la corona.

“Tumepata ushindi wa mabao mengi na mashabiki wamefurahi lakini siyo kwa timu za Tanzania lakini kwa ukanda mzima na hata Zambia niliona kitu kama hicho kwa timu inayopata ushindi wa mabao mengi na kucheza soka nzuri mashabiki wanafurahi kwa kuwa wanapenda burudani,“ alisema.

Aidha, Sven alisema kabla ya mchezo huo, alimwambia Kocha Msaidizi, Sulemani Matola kuwa watacheza soka la kujituma muda mwingi, wamiliki mpira kuliko wapinzani na kushambulia kwa kushitukiza.

Simba inaendelea kuongoza ligi ikiwa na pointi 75 na kuicha Azam kwa pointi 17 baada ya jana kutoka suluhu na Yanga ambayo nayo imeachwa kwa pointi 19.

MABINGWA wa Ligi Kuu Tanzania Bara, Simba wametajwa katika tetesi ...

foto
Mwandishi: Mwandishi Wetu

Post your comments

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi