loader
Dstv Habarileo  Mobile
Picha

Bocco: Kujituma ni siri ya ushindi

NAHODHA wa Simba, John Bocco, amesema kufuata maelekezo ya kocha na kujituma ni siri iliyowawezesha kuibuka na ushindi wa mabao 3-0 dhidi ya Mwadui FC katika mchezo uliofanyika kwenye Uwanja wa Taifa Dar es Salaam.

Mchezo huo wa Ligi Kuu Tanzania Bara ni wa pili kwa Simba baada ya ligi kusimama kutokana na janga la corona, umewafanya kufikisha pointi 75 na kuzidi kuukaribia ubingwa waliopania kutetea kwa mara ya tatu mfululizo.

Akizungumza Dar es Salaam jana, Bocco alisema matarajio yao ni kupata ushindi kwenye kila mchezo na matokeo hayo yamezidi kuwajenga kisaikolojia kuelekea kwenye michezo mingine.

“Tulicheza kwa juhudi kwa kufuata maelekezo ya kocha wetu na ushindi huu umetujenga kisaikolojia kuelekea kwenye michezo inayokuja ambayo tunajua itakuwa na ushindani kulingana na mazingira ya msimamo wa ligi ulivyo,” alisema.

Bocco ambaye kwenye mchezo huo alifunga bao moja, alisema Mwadui walionesha ushindani mkubwa, ingawa wao walitumia maarifa na akili kwa kutambua uwezo wa wapinzani na kuwashambulia kwa kushitukiza, mbinu ambayo iliwanufaisha na kuibuka na ushindi.

Pia alisema kwenye mchezo huo waliingia wakiwa na dhamira ya kupata ushindi kwa lengo kuwapa raha mashabiki kutokana na matokeo waliyopata kwenye mchezo uliopita dhidi ya Ruvu Shooting ya sare 1-1, mchezo uliofanyika kwenye uwanja huo huo.

foto
Mwandishi: Tuzo Mapunda

Post your comments

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi