loader
Dstv Habarileo  Mobile
Picha

Maxime: Wachezaji walikosa umakini

KOCHA wa Kagera Sugar, Mecky Maxime, amesema kukosekana kwa umakini wa kumalizia pasi za mwisho kwa washambuliaji wa kikosi chake, kulichangia kufungwa mabao 2-0 na Namungo FC.

Mchezo huo wa Ligi Kuu Tanzania Bara ulichezwa juzi kwenye Uwanja wa Ruangwa mkoani Lindi, ambapo wenyeji Namungo wamezidi kuendeleza ushindi wakiwa nyumbani, matokeo yanayowafanya kufikisha pointi 54 na kukoleza mbio za kuwania nafasi ya pili kwenye msimamo wa ligi inayotolewa macho na timu za Azam FC na Yanga.

Akizungumza jana, Maxime alisema mchezo huo ulikuwa mzuri na walitengeneza nafasi nyingi ambazo safu yake ya ushambuliaji ilishindwa kuzitumia na kuwapa nafasi wapinzani wao kuwafunga mabao kirahisi.

“Nawapa pole wachezaji wangu wote kwa matokeo haya, tulicheza vizuri na tulitengeneza nafasi nyingi ambazo kama umakini ungeongezeka kwa washambuliaji tungepata ushindi kwenye mechi hiyo, lakini badala yake tuliwapa nafasi wapinzani kutufunga mabao rahisi na kumaliza mchezo,” alisema Maxime.

Kocha wa Namungo FC, Hitimana Theiry, alisema waliingia kwenye mchezo huo kwa dhamira ya ushindi baada ya kupata hasira za kupata sare ya 2-2 kwenye mechi iliyopita dhidi ya Coastal Union.

“Sio jambo la kushangaza kama waliweza kutufunga kwao kwa nini sisi tusiwafunge kwetu, hilo ni la kwanza, lakini pili tuliingia kwenye mchezo kwa dhamira ya kupata ushindi kufuta hasira tuliyoipata kwenye mchezo uliopita dhidi ya Coastal” alisema Thiery.

Kwenye mchezo huo, ushindi wa kikosi hicho ulipatikana kupitia mabao yaliyowekwa kimiani na mchezaji Hashimu Manyanya na Reliants Rusajo ambaye amefikisha mabao 12 na kuzidi kumkimbiza Meddie Kagere wa Simba anayeongoza kwa mabao 19.

Kagera Sugar wanasalia kwenye nafasi ya tisa ya msimamo wa ligi kwa pointi 41 baada ya kucheza michezo 30 sawa na Namungo wanaoshika nafasi ya nne wakiwa na pointi 54.

MABINGWA wa Ligi Kuu Tanzania Bara, Simba wametajwa katika tetesi ...

foto
Mwandishi: Tuzo Mapunda

Post your comments

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi