loader
Dstv Habarileo  Mobile
Picha

Masharti ya corona yaanza kulegezwa

TAASISI za dini nchini zimetakiwa kuandaa mikakati mbalimbali ya kudhibiti maambukizi ya virusi vya corona, wakati maeneo ya ibada yakitarajiwa kufunguliwa mwishoni mwa mwezi huu.

Maagizo hayo yalitolewa katika mkutano wa Baraza la Mawaziri uliokuwa chini ya mwenyekiti wake, Rais Paul Kagame, uliofanyika Juni 16, mwaka huu.

“Maeneo ya ibada yataendelea kufungwa, wakati huu wanatakiwa kufanya uwekezaji wa kujikinga na virusi hivyo kwa kuweka mikakati ya kujilinda kabla ya kufungua maeneo hayo siku 15 zijazo,” ilisema sehemu ya taarifa hiyo.

Maeneo ya ibada yamefungwa tangu Machi mwaka huu. Baraza la Mawaziri pia limefanya uamuzi wa kufungua shughuli za ndoa katika maeneo ya ibada lakini watu wanaoruhusiwa kuhudhuria wasiozidi 30.

Taarifa iliyosainiwa na Waziri Mkuu, Edouard Ngirente, ilisema shughuli za maziko zitaendelea kufanyika kwa kuhudhuriwa na idadi ya watu wasiozidi 30.

Mawaziri hao pia wameruhusu hoteli kupokea wageni, mikutano na makongamano pamoja na kuruhusu watalii wa ndani na wa nje watakaotumia ndege ndogo zilizoruhusiwa.

JUMUIYA ya Afrika Mashariki (EAC) imewatoa hofu wananchi wa jumuiya ...

foto
Mwandishi: KIGALI

Post your comments

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi