loader
Dstv Habarileo  Mobile
Picha

YANGA haijakata tamaa

LICHA ya kupunguzwa kasi katika mbio za kuwania nafasi ya pili ya Ligi Kuu Tanzania Bara baada ya kutoka suluhu na Azam juzi, kocha wa Yanga, Luc Eymael hajakata tamaa.

Yanga ilitoka sare ya bila kufungana na Azam katika mchezo wa ligi hiyo uliopigwa kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam juzi na hivyo kupunguzwa kasi katika mbio zake hizo.

Sare hiyo kiujumla imezidi kutoa nafasi kwa Simba kuukaribia ubingwa huo baada ya Jumamosi kuifunga Mwadui ya Shinyanga kwa mabao 3-0 na kufikisha pointi 75 na kuendelea kutamba kileleni mwa msimamo wa ligi hiyo inayoshirikisha timu 20.

Eymael alisema kuwa pointi mbili walizopitwa na Azam, kamwe haziwezi kumpa presha, kwani bado ana michezo nane, ambayo ameahidi kushinda yote na kumaliza katika nafasi hiyo ya pili.

Kimsimamo, Azam wako katika nafasi ya pili wakiwa na pointi 58, mbili zaidi ya Yanga ambao wote kila mmoja amecheza mechi 30.

Alisema kuwa timu yake imepata matokeo ya sare kwenye michezo miwli dhidi ya JKT Tanzania kwa kufungana bao 1-1 kabla ya kutoka suluhu dhidi ya Azam, ambapo alisisitiza kuwa hayo ni matokeo ya kawaida katika mchezo.

“Siwezi kukata tamaa ya kupigania nafasi ya pili, kwani uwezo tunao tunapishana kwa pointi mbili dhidi ya Azam wanaoshika nafasi hiyo, sina presha kwani michezo iliyobaki tutafanya vizuri,“ alisema Eymael.

Yanga wako katika nafasi ya tatu katika mbio hizo za kuwania taji la Ligi Kuu ya Tanzania Bara na imepania kuondoa Azam katika nafasi hiyo ya pili, huku ikiwa imekata tamaa ya ubingwa baada ya kupitwa na Simba kwa pointi 19.

MABINGWA wa Ligi Kuu Tanzania Bara, Simba wametajwa katika tetesi ...

foto
Mwandishi: Tuzo Mapunda

Post your comments

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi