loader
Dstv Habarileo  Mobile
Picha

Wanasiasa wapongeza hotuba ya Rais mpya

BAADHI ya viongozi wa vyama vya siasa wamesifi a hotuba ya Rais mpya, Evariste Ndayishimiye na kueleza kuwa, ametoa fursa nzuri kwa vyama vyote vya siasa kupeleka mawazo yao serikalini kwa ajili ya maendeleo ya nchi hiyo.

Mwenyekiti wa chama cha APDR, Gabriel Banzawitonde, amepongeza hotuba hiyo na kueleza kuwa, vyama vyote vya siasa vinatakiwa kuheshimu sheria na serikali iliyopo madarakani na kuwasilisha mawazo yao kwa maendeleo ya nchi kama alivyosema Rais huyo.

“Serikali ina sheria na taratibu zake ambazo lazima ziheshimiwe na wote,” alisema.

Naye msemaji wa chama cha CNDD, Gaspard Kobako, alisema vyama vya siasa vina haki kuwasilisha maoni yao kidemokrasia.

“Hatulazimishwi kukubali maoni mbalimbali ya vyama vya siasa, kwani tuko katika ushindani,” alisema na kuongeza kuwa mawazo mengi ambayo yamekuwa yakitolewa na vyama hivyo yamekuwa na lengo la kuonesha kuwa serikali inafanya vibaya, hivyo watakuwa makini kuchuja mawazo yanayofaa na yasiyofaa.

Baada ya kuapishwa wiki iliyopita katika sherehe zilizofanyika katika viwanja vya Ingoma katika jimbo la Gitega, Rais Ndayishimiye alisema vyama vya upinzani havitakuwa na nafasi katika serikali kama havitaikubali serikali iliyopo madarakani.

Alisema kama vikiiunga mkono serikali hiyo iliyochaguliwa na wananchi, atasikiliza mawazo yao pamoja na ya asasi za kiraia kwani, wananchi wote wa Burundi ni sawa mbele ya sheria na yeye yuko kusimamia sheria.

JUMUIYA ya Afrika Mashariki (EAC) imewatoa hofu wananchi wa jumuiya ...

foto
Mwandishi: BUJUMBURA

Post your comments

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi