loader
Dstv Habarileo  Mobile
Picha

Kongamano la michezo Jumamosi

KAMATI ya Olimpiki Tanzania (TOC) imeandaa kongamano kubwa la michezo litakalofanyika Jumamosi kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam, ambalo litajadili athari za janga la virusi vya corona katika michezo nchini.

Makamu wa Rais wa Kamati ya Olimpiki Tanzania (TOC), Henry Tandau amesema jijini Dar es Salaam jana kuwa kongamano hilo litashirikisha viongozi wa michezo wa mashirikisho, ambayo yako katika mfumo wa Olimpiki pamoja na waandishi wa habari za michezo nchini.

Tandau amesema walitaka kualika watu wengi, lakini wamealika 60 ili kuhakikisha wanazingatia umbali wa meta moja kati ya mtu na mtu wakati wa kongamano hilo muhimu.

Amesema awali walitakiwa kuwa na Siku ya Olimpiki, ambayo ilipangwa kufanyika Juni 21, lakini kutokana na corona hawakufanya na badala yake wataendesha kongamano hilo, ambalo litakuwa na manufaa kwa michezo nchini.

Akielezea mada zitakazotolewa siku hiyo, Tandau alisema ni pamoja na athari za virusi vya corona kwa michezo nchini, hasa maandalizi ya Michezo ya Olimpiki ya 2020.

Nyingine ni changamoto na fikra za mipango ya michezo baada ya janga la ugonjwa wa covid-19, pamoja na mchango wa michezo kwa muhimili wa maendeleo.

Michezo ya Olimpiki ya 2020 ilipangwa kufanyika Tokyo, Japan kuanzia Julai mwaka huu kabla ya kuahirishwa kwa mwaka mmoja, na sasa itafanyika Julai 23 hadi Agosti 8, 2021.

Hadi sasa wanariadha wawili wa Tanzania, Alphonce Simbu na Failuna Abdi ndio waliofuzu kushiriki Michezo ya Olimpiki ya 2020 Tokyo, huku ndondi wakijaribu lakini hawajapata baada ya kushindwa katika michezo ya Afrika iliyofanyika Senegal.

MABINGWA wa Ligi Kuu Tanzania Bara, Simba wametajwa katika tetesi ...

foto
Mwandishi: Mwandishi Wetu

Post your comments

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi