loader
Dstv Habarileo  Mobile
Picha

KMC tayari kuimaliza Biashara United

KOCHA Msaidizi wa timu ya Manispaa ya Kinondoni (KMC), Habib Kondo amesema timu yake imejipanga vyema kuhakikisha inaibuka na ushindi katika mchezo wake wa Ligi Kuu dhidi ya Biashara United. Mchezo huo unatarajiwa kuchezwa leo katika Uwanja wa CCM Karume mkoani Mara.

Akizungumza na gazeti hili wakati wa mazoezi yao kwenye uwanja wa CCM Kirumba jana, Kondo amesema kwa sasa lengo kubwa kwao ni kuhakikisha wanashinda michezo yao iliyobaki.

Kocha huyo wa zamani wa Alliance FC na Maji Maji FC alisema timu yake haipo katika nafasi nzuri, hivyo watapambana kuhakikisha wanakwepa kushuka daraja.

‘’Lengo ni kushinda mechi zote kwani kwa sasa bado hatupo katika nafasi nzuri, tutaendelea kupambana ili kufanya vyema,’’ amesema Kondo.

Kuelekea mchezo wa leo dhidi ya Biashara United, Kondo amesema mchezaji wake, James Msuva ataukosa mchezo huo kutokana na maumivu ya misuli.

Alisema baada ya mechi dhidi ya Biashara United, timu yake itarejea jijini Mwanza kujipanga kwa ajili ya mchezo wao dhidi ya Kagera Sugar utakaochezwa katika Uwanja wa Kaitaba mjini Bukoba.

Katika msimamo wa ligi hiyo, KMC ipo katika nafasi ya 12 ikiwa na alama 36 baada ya michezo 30. KMC imeshinda mechi 10, ikitoka sare mara sita na imepoteza mechi 14, huku ikifungwa mabao 34 na kufunga mabao 28.

MABINGWA wa Ligi Kuu Tanzania Bara, Simba wametajwa katika tetesi ...

foto
Mwandishi: Alexander Sanga, Mwanza

Post your comments

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi