loader
Dstv Habarileo  Mobile
Picha

Ilani ya CCM imeleta maendeleo Peramiho

JENISTA Mhagama ni miongoni mwa wanasiasa wanawake aliyejizolea umaarufu usiochuja na sifa kubwa nchini kutokana na uwezo mkubwa wa uongozi naaouonesha katika nyanja mbalimbali.

Kwa sasa ni Mbunge Mstaafu wa Jimbo la Peramiho lililopo mkoani Ruvuma. Kutokana na uchapakazi wake, Rais John Magufuli alimteua kuwa Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Walemavu).

Ni kwa msingi huo, wananchi mbalimbali jimboni Peramiho wanamkumbuka na kumwelezea Mbunge Mstaafu Jenesta kama alama ya maendeleo isiyopaswa kufutika kwani ameutangaza vema Mkoa wa Ruvuma.

“Jenista ni ‘icon’ (alama) ya Ruvuma; ameutangaza vema Mkoa wa Ruvuma kwa kutuletea maendeleo tena amekuwa mstari wa mbele kufuatilia miradi ya maendeleo na kuleta pesa. Tunampongeza sana kwa ujasiri huo maana ni viongozi wachache wakiwamo hata wanaume, wenye uwezo na upendo kama huo,” anasema mkazi wa Songea, Violeth Haule.

Anasema uwezo wa Jenista kujibu hoja bungeni na namna alivyowapenda na kuwahudumia wanajimbo wake, ni mambo yanayowafanya Wanaperamiho kuzidi kumpenda kila kukicha kwa amekuwa mfano bora wa kuigwa.

“Huyu mama amekuwa na roho ya umama na uongozi kwelikweli; anajitolea kwa hali na mali kusaidia maendeleo jimboni mwake na amekuwa mwanasiasa mwenye heshima kwa wakubwa na wadogo… Kweli ametufurahisha sana kwa utumishi wake.”

Huyo ndiye Jenista Mhagama; ambaye kutokana na umakini katika utumishi wake kwa umma, amewahi kuwa Mwenyekiti wa Bunge 2010 -2015 na Katibu wa Wabunge wa Chama Cha Mapinduzi Tanzania Bara. Ni Mbunge anayetajwa kuwa na uwezo mkubwa katika kujenga, kuimarisha na kulinda uhusiano mwema baina yake, wananchi, wabunge wenzie hata nje ya mkoa, wanachama, madiwani na viongozi wengine.

Mkazi wa Mgazini katika Kata ya Kilagano, Dickson Ngo- nyani anas- ema, Jeni- sta ni mwanamke aliyethubutu na kuweza kuivusha Peramiho kwa kupeleka miradi mingi ya maendeleo na kuitekeleza kwa vitendo.

Ngonyani anasema: “Mama Mbunge amesaidia kufuatilia umeme kiasi kwamba, mpaka sasa karibu vijiji vyote vina umeme pia, amesaidia kuhakikisha kila kijiji kinapata zahanati na huduma za afya zimeboreshwa. Amepambana kuhakikisha afya za wananchi zinaendelea kuimarika.”

“Anatumia maisha yake ya kibunge kujiweka karibu na wapiga kura wake; ametekeleza ilani kwa vitendo kwa kushirikiana na wananchi wake akipita mara kwa mara katika kata na vijiji jimboni kwake kusikiliza kero za wapiga kura na kuzitatua; ndiyo maana tunamuomba aendelee kutusaidia ili atutatulie kero ya maji,” anasema.

Kuhusu miundombinu katika shule, Jenista mwenyewe anasema: kwa kushirikiana na serikali na wadau mbalimbali wa elimu jimboni Peramiho, pia wamekarabati miundombinu ya vyoo, nyumba za walimu na nyumba za waganga.

“Tumeweka sola za umeme mkubwa katika shule za sekondari 16, mabweni na nyumba za waganga na tumeweka sola zahanati 13 na nyumba za wahudumu wa afya katika zahanati zote 13,” anasema.

Anapozungumzia umeme kutoka Wakala wa Nishati Vijiji (REA), anasema umefika kila kijiji katika njia kuu na vijiji vyote vya Jimbo la Peramiho huku baadhi ya maeneo yakiendelea kufanyiwa kazi.

Diwani wa Kata ya Mpitimbi, Issa Kindamba anasema katika kipindi chake cha ubunge kilichomalizika hivi karibuni, Jenista amechangia miradi mbalimbali ya maendeleo ikiwa ni pamoja na kutoa mifuko ya saruji zaidi ya 300 kwa ajili ya ujenzi wa zahanati ya Kijiji cha mpitimbi A na ujenzi wa vyumba viwili vya madarasa na ofisi moja ya walimu katika Shule ya Msingi Humbaro.

Ujenzi huo uliofadhiliwa na Mbunge Jenista umegharimu Sh milioni40 milioni huku akichangia saruji katika Shule ya Mbwambwasi, na ukarabati wa zahanati ya Kijiji Lipaya na mchango wa vifaa vya michezo ikiwemo jezi na mpira. Kwa mujibu wa uchunguzi kupitia vyanzo mbalimbali, kabla Mhagama hajaingia madarakanai kama Mbunge wa Peramiho, jimbo hilo lilikuwa na shule mbili za sekondari ambazo ni Maposeni na Mpitimbi.

“Kwa sasa kila kata ina shule ya sekondari na kata mbili zina shule mbili za sekondari,” kinasema chanzo kimoja na kuongeza: “Hapakuwa na shule ya kidato cha tano na sita, lakini sasa tuna shule 2 za kidato cha tano na sita za Mpitimbi na Maposeni ambazo zimepanda hadhi… Tunatarajia kujenga shule ya sekondari ya wasichana ya kidato cha tano na sita.”

Mintarafu suala la elimu, Mbunge Jenista mwenyewe anasema: “Tulikuwa hatujaimarisha elimu ya ufundi, lakini kwa sasa tumetumia fedha za Kitanzania takriban Sh milioni 600 kuimarisha Chuo cha Maendeleo ya Jamii Muhukuru ili kuongeza ujuzi na kuwasaidia vijana kutumia ujuzi kujiajiri hivyo, tumekarabati karakana na bweni.” “Tunatarajia kuomba fedha za ukarabati wa awamu ya pili ili kukarabati pia Chuo cha Maendeleo ya Jamii Mlale.”

Anasema kupitia Serikali zaidi ya vijana 600 wamenufaika na kozi maalum ya ufundi stadi bure katika Chuo cha Ufundi Peramiho na sasa wapo katika soko la ajira.

Anasema: “Katika kipindi hiki, tumejenga mabweni katika sekondari za kata. Tumezijengea madarasa mapya shule zetu kongwe za msingi kongwe zikiwemo za Lunduzi, Parangu, Liganga, Humbaro, Mpandangindo, Mnyonga, Ndogosi, Muungano, Namatuhi, Liula, Mipeta, Matama, Lunyele, Mkondo wa Shule Jenista, Nakawale, Kivukoni na Urambo.”

Katika kata hiyo uchunguzi umebaini kuwa, mbunge huyo amechangia fedha binafsi zaidi ya Sh milioni 53 kwa shughuli na miradi mbalimbali. Aidha, Mbunge amesaidia upatikanaji wa fedha za ujenzi wa Hospitali ya Wilaya ya Songea Sh bilioni 1.5 na tayari ujenzi umeshaanza hivyo tunamshukuru sana kwa misaada na maendeleo ambayo ametupatia kwani tunaona jitihada zake.

Athuman Ibadi, mkazi wa Lilai anasema: “Kweli Peramiho tunayo bahati tunayopaswa kuilinda; huyu mbunge ni bahati kwetu; ametekeleza zaidi ya alivyoahidi; amewajengea Daraja la Magwamila, barabara sasa zinapitika na amewachimbia visima sasa wanapata maji safi na salama; Mungu atupe nini zaidi!” Katibu Chama Cha Mapinduzi (CCM), Wilaya Mohamed Lawa anasema, michango ya Jenista kama Mbunge kwa wananchi na chama imekuwa ya kutukuka na wanajivuna kwa kuwa walikuwa na Mbunge mwenye hofu ya Mungu na anayepambana kwa ajili ya wananchi wake.

“Ametoa pikipiki 16 kukichangia chama ngazi ya kata zenye thamani ya Sh 36,800,000 na baskeri 132 kila tawi zenye thamani Sh 22,440,000,” anasema Lawa akishuhudia uchapakazi wa Jenista kwa wananchi wa jimbo lake.

Anaongeza: “Ametoa mabati zaidi ya 800 katika misikiti na makanisa; amechimba visima virefu vyenye urefu wa mita 120-150 katika vijiji 22 na amesapoti bati 150 za ujenzi wa zahanati ya Mhepai.”

“Uongozi wake ni wa mfano na amekuwa mstari wa mbele kuhamasisha maendeleo; amejitoa kweli kweli kusaidia wananchi wake, hata sisi viongozi wake tunavutiwa na jitihada zake, hivyo tunamwomba aendelee kuwasaidia wapiga kura kama Ilani yetu inavyosema,” anasema Lawa.

Diwani wa Kata ya Mhukuru, Simon Kapinga, anasema Jenista ni kiongozi mwenye juhudi katika kufuatilia utekelezaji wa miradi ya maendeleo na wanajivuna kuwa naye.

“Katika kata yetu, ametoa mabati 200 na mifuko 72 ya saruji kwa ajili ya kupaua katika Shule ya Msingi Lihuhu, mabati 104 kwa ajili ya Ofisi ya Kijiji cha Makwaya na pia, amechangia kitanda cha kujifungulia wajawazito na shuka na ununuzi wa betri ya sola katika sekondari ya kata,” anasema.

Anaongeza: “Hivi karibuni ametugawia vifaa vya kujilinda dhidi ya corona zikiwemo ndoo na sanitaiza ambazo zimesambazwa kwenye taasisi ikiwemo Kituo cha Afya Mhukuru, katika shule mbalimbali, Chuo cha Maendeleo na taasisi za dini ambapo mchango binafsi wa mbunge ni zaidi ya Sh milioni 20.”

Kuhusu huduma za afya jimboni Peramiho, anasema: “Nilipoanza kulikuwa na zahanati 10, lakini sasa tuna zahanati karibu kila kijiji isipokuwa baadhi ya zahanati zinakamilisha ujenzi zikiwa Mpitimbi A, Nyamechini, Mipeta, Matama Mchepai.”

“Aidha, nilipoanza utumishi katika jimbo hili, kulikuwa na kituo cha afya kimoja; kwa sasa tumepata fedha za kukamilisha vituo vya afya vitano.” “Kituo cha Afya cha Muhukuru kimekamilika na kimeanza kufanya upasuaji; Magangura na Matimimila viko katika hatua za ujenzi; Lugagara na Nakahegwa na Lipaya vimeanza kufanya kazi bila upasuaji, Mpigi kimekamika kinangoja vifaa.”

Mbali na hayo Jenista anasema: “Kwa kushirikiana na wanananchi na wadau mbalimbali wa maendeleo jimboni Peramiho, tumeanzisha miradi ya kiuchumi kwa vijana na akina mama ikiwa ni pamoja na kutoa majiko ya gesi 40 kwa mama lishe.”

“Aidha, tumetoa viti mwendo 60 kwa watu 60 wenye ulemavu, tumetoa kompyuta kwa sekondari 9 na vishikwambi 10 kwa shule za msingi. Kuhusu huduma za maji, Jenista anasema Mbunge Mhagama anasema: “Mradi mkubwa wa maji mtiririko kutoka Lugagara Zomba, Mgazini, Maposeni, Peramiho A na B na Lundusi umekamilika katika vijiji viatu na sasa kisima cha Bruda cha Peramiho B kinawekewa miundombinu kupeleka maji peramiho B na Lundusi.”

Anaongeza: “Visima virefu vya maji 22 vimechimbwa katika vijiji 22 vyenye urefu wa zaidi ya mita 150 kwenda chini kusaidia upatikanaji maji.”

Mradi mkubwa wa maji Kijiji cha Liula umekamilika na ukarabati wa visima vifupi katika vijiji umekamilika mradi wa maji wa ushirikiano na wamisionari wa Parokia ya Ndongosi.

Mwenyekiti wa CCM Wilaya ya Songea Mary Due anasema Jenista Mhagama amefanya kazi kubwa kuwaletea maendeleo wanajimbo huku akijitahidi kutoa msaada wa vifaa vya Viwandani saruji, mabati na hata pesa taslimu kwa ajili ya maendeleo ya jamii hasa ujenzi wa shule za msingi, sekondari, zahanati, ofisi za vijiji na kuchangia shuguli za chama.

Alipoulizwa kwa kifupi anamwelezeaje Jenista, Mary anasema: “Jenista ni mchapakazi anayejitoa kushirikiana na kuwa karibu na wapiga kura wake na amekuwa na uhusiano mzuri na viongozi wa chama na wapiga kura wake hali ambayo imejenga imani, upendo na heshima kubwa kwa chama, jimbo hilo na Taifa kwa jumla.”

UCHAGUZI Mkuu umekaribia, wananchi katika maeneo mbalimbali ikiwemo majimboni na ...

foto
Mwandishi: Mwandishi Wetu

Weka maoni yako

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi