loader
Dstv Habarileo  Mobile
Picha

Simba yaukaribia ubingwa

SIMBA imeendelea kuukaribia ubingwa wa Ligi Kuu Tanzania Bara msimu wa mwaka 2019/2020 baada ya jana kuibuka na ushindi wa mabao 2-0 dhidi ya Mbeya City kwenye Uwanja wa Kumbukumbu ya Sokoine, Mbeya.

Katika mchezo huo, nahodha wa Simba John Bocco ndiye alikuwa mwiba mkali baada ya kufunga mabao yote mawili na kuifanya timu hiyo kuendelea kufanya vizuri katika mbio zake za kutetea ubingwa.

Bocco alifunga bao la kwanza dakika tano tangu kuanza kwa mchezo huo akimalizia pasi safi iliyochongwa na Clatous Chama kabla ya kupachika bao la pili katika dakika ya 54, akipokea pasi iliyotengenezwa na kiungo Francis Kahata.

Bocco sasa amefikisha mabao saba aliyofunga katika ligi hiyo, huku Simba ikiwa na pointi 78 baada ya kucheza michezo 31, na inahitaji pointi tatu ili ifikishe 81, ambazo haziwezi kufikiwa na timu yoyote ile baada ya Azam jana kufungwa na Kagera Sugar 1-0 kwenye Uwanja wa Kaitaba, Bukoba.

Kabla ya mchezo huo, Azam ilikuwa na pointi 58 na kama isingefungwa ingekuwa na uwezo wa kufikisha pointi 82 kama ingeshinda mechi zake zote zilizobaki, lakini sasa ina uwezo wa kufikisha pointi 79 tu.

Simba sasa inaweza kutangaza ubingwa ikiwa mkoani Mbeya, andapo Jumapili itaibuika na ushindi dhidi ya Tanzania Prisons kwenye Uwanja wa Kumbukumbu ya Sokoine.

Washindi waliuanza mchezo huo wa Mbeya kwa kasi na kuonekana wakiwa na shauku ya kufunga, licha ya kucheza bila mshambuliaji wao hatari, Meddie Kagere, ambaye hadi sasa ana mabao 19. Hadi timu zinaenda mapumziko, Simba walikuwa kifua mbele kwa bao kwa bao 1-0.

Matokeo ya michezo mingine iliyopigwa jana; Alliance walitoka sare ya kufungana bao 1-1 dhidi ya JKT Tanzania mchezo uliofanyika kwenye Uwanja wa Nyamagana, Mwanza, Biashara United waliibuka na ushindi wa mabao 4-0 dhidi ya KMC.

Jana usiku, Yanga ilimenyana na Namungo FC kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam na kama ikishinda itaitoa Azam katika nafasi ya pili, kwani itafikisha pointi 59.

MABINGWA wa Ligi Kuu Tanzania Bara, Simba wametajwa katika tetesi ...

foto
Mwandishi: Tuzo Mapunda

Post your comments

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi