loader
Dstv Habarileo  Mobile
Picha

Nyota ya Samatta yazidi kung’ara

SHIRIKISHO la Soka Barani Afrika (CAF), limemtaja Nahodha wa Taifa Stars, Mbwana Samatta, kama miongoni mwa wachezaji wanne wakali wa mabao ya vichwa kutoka Afrika.

Kupitia ukurasa rasmi wa mtandao wa kijamii wa Twitter, CAF imewataja wengine wa zamani kuwa ni Didier Drogba (Ivory Coast/Chelsea) Hossam Hassan (Misri/Al Ahly) na Flavio Amado (Angola/ Petro Atletico), kuwa ndio wachezaji hatari kwa magoli ya vichwa.

Samatta aliwekwa kwenye orodha hiyo kutokana na uwezo wake mkubwa wa kufunga mabao ya vichwa tangu akiwa TP Mazembe ya DRC Congo, ambako aliibuka mfungaji bora wa michuano ya Ligi ya Mabingwa Afrika mwaka 2015 akiwa na mabao saba na kujumuishwa katika kikosi bora cha Afrika.

Si hivyo tu, Samatta aliendelea kufunga hasa mabao ya vichwa baada ya kutua Genk mwaka 2016, ambako alifunga mabao zaidi ya 15 ya vichwa katika michezo mbalimbali ikiwamo ya Ligi Kuu ya Ubelgiji.

Samatta aliteka hisia za watu baada ya kufunga bao la kichwa katika mchezo wa Ligi ya Mabingwa Ulaya dhidi ya Liverpool, ambalo lilichaguliwa na klabu ya Genk kuwa bao bora la msimu uliopita la klabu hiyo.

Mshambuliaji huyo wa zamani wa TP Mazembe, aliendelea kuuwasha moto huo wa mabao ya vichwa akiwa Aston Villa, ambako alifunga bao la kichwa cha kupiga mbizi kama samaki anayeogelea Ziwa Victoria katika mchezo wa fainali ya Carabao Cup dhidi ya Manchester City.

Sambamba na kumtaja Samatta na wachezaji wengine, CAF inatambua uwapo wa nyota wengine ambao hata hivyo hawakuorodheshwa na kuacha zoezi la kuwataja wengine kwa mashabiki wa ukurasa wao wa Twitter.

BAADA ya Namungo FC ...

foto
Mwandishi: Rahimu Fadhili

Post your comments

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi