loader
Dstv Habarileo Mobile
Picha

Ubaharia uboreshwe kuchangia pato la taifa

TANZANIA ni kati ya nchi zilizoridhia mikataba ya uboreshwaji wa maslahi ya fani ya ubaharia lengo kubwa likiwa kuwawezesha mabaharia kutambua na kufurahia thamani ya kazi hiyo.

Jana ilikuwa siku ya kimataifa ya maadhimisho ya siku ya mabaharia duniani inayoadhimishwa kila Juni 25, Shirika la Wakala wa Meli nchini (Tasac) liliratibu maadhimisho hayo nchini.

Tasac iliwakutanisha wadau wa ubaharia kuzungumzia masuala ya fani hiyo kikao kilichoshirikisha waandishi wa habari. Kwa mujibu wa Chuo cha Ubaharia Dar es Salaam (DMI, kuna Watanzania mabaharia 5,300 waliohitimu katika chuo hicho.

Wapo wanaofanya kazi ndani na nje ya nchi. Mabaharia walio nje ya nchi wanafanya kazi Abu Dhabi na Dubai, Umoja wa Falme za Kiarabu (UAE), Qatar na nchi nyinginezo.

Hivyo huenda mabaharia wako wengi zaidi kwa kuwa wapo walioenda nje ya nchi bila kupitia chuoni DMI, chuo kikubwa kwa Ukanda wa Afrika Mashariki na Kati kinachotambulika kama chuo cha umahiri kwa nchi wanachama wa jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC).

Hii inamaanisha wahitimu wa chuo hicho wanaweza kufanya kazi nchi yoyote hata nje ya Afrika na kupata malipo kwa fedha za kigeni. Serikali kupitia DMI iwatafutie mabaharia kazi nje ya nchi hata kama wakikatwa asilimia kadhaa kutoka katika mishahara wanayopata.

Fedha za kigeni watakazolipwa zitakuwa mchango wao kwa pato la taifa. Zipo nchi zinazouza mabaharia wao nchi nyingine.

Wapo mabaharia wanaziletea familia zao fedha hizo za kigeni ingawa hakuna taarifa zao rasmi. Chini ya mpango wa DMI wa kutafuta taarifa za mabaharia wote nchini hao pia watajulikana walipo na kujua kiasi gani cha dola wanaingizia nchi kwa njia hiyo ya kusaidia familia zao.

Jitihada za Rais John Magufuli za kujenga meli hasa mikoa ya Kanda ya Ziwa zinaweza nazo kutanua wigo wa kazi za ubaharia hapa nchini.

Lazima uwepo wa meli hizo uwajengee uwezo mabaharia wa kesho kwa kuwapatia fursa thabiti mabaharia chipukizi kujipatia uzoefu wa kazi.

Hatua hiyo itaimarisha utendaji kazi wao na pia ni vema fursa za ubaharia zikatangazwa ili kila Mtanzania mwenye sifa azichangamkie sawia.

DMI fanyieni haraka maboresho ya mitaala ili kuzalisha wataalamu wa kufanya kazi meli za utafiti wa gesi au mafuta Watanzania wawe wanufaika wakubwa tofauti na meli za utafiti wa gesi Mtwara kutawaliwa na mabaharia kutoka nchi nyingine za Afrika Magharibi.

Kama serikali ilivyotangaza fursa katika madini na sekta nyingine, ubaharia kuna fursa nyingi. Ni suala la kutafuta weledi wake darasani, kwa kuwa yapo mafunzo ya muda mfupi ya miezi mitatu na ya muda mrefu pia hasa hapo DMI.

KATIKA miaka ya karibuni msimu wa mavuno kumekuwa na watu ...

foto
Mwandishi: Evance Ng’ingo

2 Comments

 • avatar
  Comfort 2020 Comfort
  03/07/2020

  Kazi yako nzuri na nilishawahi kufanya iliishia hapa 1. Kuandaa TOFAUTI 2. Kuandaa Tofari 3. Kuona 4. Kusikia 5. KUONYESHA N.K

 • avatar
  Comfort 2020 Comfort
  03/07/2020

  Kazi yako nzuri na nilishawahi kufanya iliishia hapa 1. Kuandaa TOFAUTI 2. Kuandaa Tofari 3. Kuona 4. Kusikia 5. KUONYESHA N.K

Weka maoni yako

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi