loader
Dstv Habarileo  Mobile
Picha

Yanga, Azam zaibeba Simba

BAADA ya kukamilika kwa mzunguko wa 31 wa Ligi Kuu soka Tanzania Bara, matokeo waliyopata Yanga na Azam katika michezo yao yameipa kazi nyepesi Simba kuzidi kulikaribia taji.

Kabla ya mechi hizo zilizopita, Simba ilikuwa inahesabu mechi tatu ili kutangaza ubingwa lakini juzi ilishinda mchezo wake dhidi ya Mbeya City mabao 2-0 na kufikisha jumla ya pointi 78, ilitakiwa ibakize michezo miwili kama Yanga na Azam wangeshinda mechi zao zilizopita.

Yanga ilipata sare ya mabao 2-2 dhidi ya Namungo yaliyosababisha kubakia nafasi ya tatu na kufikisha pointi 57 huku Azam FC iliyofungwa na Kagera Sugar bao 1-0 ikiendelea katika nafasi yake ya pili kwa pointi 58.

Matokeo hayo yanawapa nafasi wekundu hao wa Msimbazi badala ya kubakiza mechi mbili sasa watasubiri kushinda mchezo mmoja ujao dhidi ya Tanzania Prisons utakaochezwa Jumapili jijini Mbeya kutangaza ubingwa , ambao kama watashinda watafikisha pointi 81.

Pointi hizo hakuna timu yoyote itakayeweza kuzifikisha hata ikishinda mechi saba kila mmoja ilizobakiza.

Kwa maana hiyo, Azam inayofuatia nyuma, kama itashinda mechi zake zilizobaki itafikisha pointi 79 na Yanga itafikisha 78.

Vita itaendelea kuwepo kuwania nafasi ya pili, ambapo kuna timu tatu zilizofuatana na kutofautiana kidogo Azam, Yanga na Namungo kila mmoja ana nafasi kutegemea na nani atafanya vizuri michezo yake ijayo.

Kuanzia nafasi za katikati zinawaniwa na Coastal Union yenye pointi 48, JKT 47, Polisi Tanzania 47, Kagera Sugar 44, Biashara United 43, Tanzania Prisons 42 na Ruvu Shooting pointi 41.

Lakini timu hizo zinaweza kushushana kutegemea matokeo watakayokuwa wanapata katika michezo ijayo, watakaobweteka wanaweza kuwapisha wengine.

Mtibwa Sugar yenye pointi 37, Mwadui 37, KMC 36, Ndanda 35, Lipuli 34 na Alliance 33 zimekuwa zikijikongoja taratibu kutoka chini na kuanza kupanda juu ila kazi ipo kubwa mbele yao kwa sababu hawana uhakika wa kuwa salama. Kati ya timu hizo, Lipuli imetoka juu na inazidi kushuka isipojitahidi hali itakuwa mbaya.

Kwa upande wa Alliance, licha ya kujitahidi kupambana katika michezo miwili iliyopita na kupata pointi nne, bado ina kazi ya kujiondoa kwenye mstari wa kushuka daraja.

Hali sio shwari kwa Mbeya City iliyotoka kupoteza michezo miwili iliyopita kwenye uwanja wake wa nyumbani ina pointi 30 katika nafasi ya 18, inaweza kuwa na nafasi kama itajitahidi michezo iliyobaki.

Mbao inashika nafasi ya 19 kwa pointi 26 na kila msimu imekuwa ikinusurika kushuka, hivyo timu hiyo pamoja na Singida inayoshika mkia kwa pointi 15, ina mtihani mzito.

BAADA ya Namungo FC ...

foto
Mwandishi: Grace Mkojera

Post your comments

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi