loader
Dstv Habarileo  Mobile
Picha

Mashabiki marufuku mechi Simba, Yanga ugenini

Serikali imezuia mashabiki katika mechi zote za timu ya Mbeya City za nyumbani na mechi za timu za Simba na Yanga nje ya Dar es Salaam. Taarifa hiyo ilitolewa kwenye vyombo vya habari Dar es Salaam jana na Kaimu Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano Serikalini wa Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Shamimu Nyaki.

Katika taarifa hiyo, serikali ilisema imefikia hatua hiyo kutokana na timu hizo kukiuka Mwongozo wa Afya Michezoni. Ilisema Mbeya City ikiwa katika Uwanja wake wa nyumbani wa Sokoine jijini Mbeya, katika mchezo wake na Simba, ilikiuka mwongozo huo kwa kuchajaza mashabiki bila kuzingatia hatua za mita moja kwa kila mtu. Ilisema katika mchezo huo, Na.310 uliochezwa juzi, mashabiki walijazana uwanjani, hivyo kukiuka Kanuni Na 2.0.2(iii) inayosisitiza kuachana kwa mita moja.

Taarifa hiyo ilisema uchunguzi umebaini kwamba wawaikilishi wa timu mwenyeji na wadau wengine ambao ndio walikuwa na dhamana ya kudhibiti mageti, hawakutekeleza majukumu yao ipasavyo.

Kwa mujibu wa taarifa hiyo, hatua hiyo inalenga kuzikumbusha klabu wenyeji, wasimamizi wa michezo na wadau wengine kote nchini kuendelea kusimamia kikamilifu Mwongozo wa Afya na taratibu nyingine katika kudhibiti ugonjwa wa Covid-19 hadi hapo utakapoisha kabisa nchini.

Pia taarifa hiyo ilisema viwanja vingi nje ya Dar es Salaam ni vidogo na wenyeji na wadau wengine wanashindwa kukabiliana na watazamaji kungia uwanjani wakati wa timu zao zinapocheza na tumu za Simba na Yanga.

Hivyo, serikali haitaruhusu mashabiki kuingia uwanjani, mechi zilizosalia kwa timu hizo nje ya Dar es Salaam hadi pale uongozi wa timu wenyeji watakapowasilisha kwa maandishi mpango makakati wao wa kudhibiti mashabiki wafuate mwongozo huo.

BAADA ya Namungo FC ...

foto
Mwandishi: Mwandishi Wetu

Post your comments

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi