loader
Dstv Habarileo  Mobile
Picha

MASTAA YANGA WAMKATAA MORRISON

MASTAA wa zamani wa Yanga wameushauri uongozi wa timu hiyo kuvunja mkataba na Benard Morrison na kumtafuta mbadala wake kwa maslahi mapana ya klabu hiyo.

Kauli hiyo ilitolewa siku moja baada ya uongozi wa Yanga kupitia kwa Kaimu Katibu Mkuu, Saimon Patrick kuandika barua ya kuoneshwa kusikitishwa na kitendo kilichofanywa na Morrison kwa kuitisha mahojiano na chombo cha habari kwenye kambi bila kufuata utaratibu.

Wakizungumza Dar es Salaam jana, nyota hao, Akida Makunda na Iddi Moshi waliojizolea sifa kwenye vikosi vya Yanga na Simba miaka ya 1990 walisema hakuna timu inayotegemea huduma ya mchezaji mmoja, hivyo waachane na Morrison.

Moshi alisema uongozi unatakiwa kufanya maamuzi magumu kwa mchezaji huyo ili iwe fundisho kwa wengine wakigeni watakaosajiliwa ili kutengeneza heshima na kukuza thamani ya timu.

Kwa upande wake, Makunda aliyewahi kuwika na timu ya Simba na Yanga kwa nyakati tofauti alisema ni wakati wa viongozi kusimamia kanuni kwa kuwa wamepewa jukumu.

BAADA ya Namungo FC ...

foto
Mwandishi: Tuzo Mapunda

Post your comments

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi