loader
Dstv Habarileo  Mobile
Picha

Pointi mezani zaibeba Dodoma FC

KLABU ya Daraja la Kwanza ya Dodoma FC imepewa ushindi wa pointi tatu na magoli matatu kutokana vurugu za mashabiki wa timu pinzani ya Mlale walipokutana mwishoni mwa wiki iliyopita.

Katika mchezo huo, mashabiki wa Mlale walimshambulia mwamuzi msaidizi namba mbili na kusababisha mchezo huo kuvunjika kutokana na maumivu.

Pointi hizo za mezani zinawapandisha Dodoma iliyokuwa nafasi ya pili hadi nafasi ya kwanza kwa kufikisha pointi 42 na kuishusha Ihefu ambayo nayo ina pointi kaa hizo, wakitofautiana katika mabao ya kufunga na kufungwa.

Dodoma imefikisha mabao 31 ya kufunga na kufungwa 10, huku Ihefu ikiwa na 27 na kufungwa 11 katika idadi ya michezo 19 kila mmoja.

“Maamuzi hayo yamekuja baada ya Kamati ya Uendeshaji na Usimamizi wa Bodi Ligi Kuu Tanzania (TPLB) kukutana katika kikao chake cha Juni 23, mwaka huu kupitia mwenendo na matukio mbalimbali,” ilisema taarifa ya Mtendaji Mkuu wa Bodi hiyo, Almas Kasongo.

Klabu ya Mlale imepigwa faini ya Sh 500,000 kutokana na vurugu hizo, huku Kocha Msaidizi, Rashid Mpenda akifungiwa miezi sita na faini ya Sh 300,000 kwa kosa la kumshambulia mwamuzi wa kati na mwamuzi msaidizi namba mbili na uwanja wao wa Majimaji ukifungiwa uwepo wa mashabiki katika mechi zote zijazo.

Katika hatua nyingine, wachezaji Lamine Moro wa Yanga na Mwinyi Kazimoto wa JKT Tanzania wamefungiwa kucheza mechi zijazo za Ligi Kuu soka Tanzania Bara.

Lamine amefungiwa mechi tatu na kutozwa faini ya Sh 500,000 kwa kosa la kumrukia mgongoni mchezaji wa JKT Tanzania, Kazimoto na mchezaji huyo kuanguka chini katika mchezo uliokutanisha timu zao mwishoni mwa wiki iliyopita mkoani Dodoma.

Pia Kazimoto amefungiwa mechi mbili kwa kosa la kuleta vurugu uwanjani katika mchezo huo. Kuhusu malalamiko ya Azam FC dhidi ya waamuzi waliochezesha mechi dhidi ya Yanga hivi karibuni, kamati hiyo ilisema imepeleka kwenye Kamati Maalum ya Waamuzi kwa ajili ya kuyapitia na kuyarudisha kwenye kikao kijacho cha Kamati ya TPLB.

BAADA ya Yanga kurejea na ...

foto
Mwandishi: Grace Mkojera

Post your comments

Tangazo

CRDB

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi