loader
Dstv Habarileo  Mobile
Picha

Morrison na muvi ya kihindi Yanga

VIONGOZI wa Yanga kwa sasa wanaumiza vichwa na matukio ya utovu wa nidhamu yanayofanywa na mchezaji wa timu hiyo, Bernad Morrison. Morrison ambaye ni raia wa Ghana ameita chombo cha habari na kufanya mahojiano kwenye kambi wakati kikosi kinafanya maandalizi ya mwisho kuelekea kwenye mchezo wa ligi dhidi ya Namungo FC.

Aidha, aligoma kusafiri na timu kwenda mkoani Shinyanga kucheza mechi za Ligi dhidi ya Mwadui FC na JKT Tanzania uliofanyika Uwanja wa Jamhuri Dodoma. Matukio yote hayo yaliyofanyika yamevunja kanuni na taratibu walizojiwekea kama klabu, ambapo amepigwa adhabu ya kukatwa Sh 1,500,000 kwenye mshahara wake kwa kuifanyia hujuma timu hiyo wakati ikielekea katika mchezo wake dhidi ya Namungo.

JEURI YA MORRISON

Mchezaji huyo aliyesajiliwa na Yanga kipindi cha dirisha dogo la usajili, aliingia kwa mkataba wa miaka miwili kama mchezaji huru, ambaye hana timu lakini ubora na uwezo wake ulionekana kuinufaisha timu hiyo, ambayo kwa muda mrefu ilikuwa ikimtafuta winga mwenye ubora.

Lakini tukio la kuwafunga bao 1-0 watani wa jadi Simba kwenye mchezo uliofanyika katika Uwanja wa Taifa Machi 8, ndio linaonekana wazi kumvimbisha kichwa mchezaji huyo na kujiona kuwa hakuna kama yeye latika klabu hiyo.

Mashabiki na wanachama huwezi kuwaambia lolote kwa Morrison kwani amekuwa gumzo hadi kwenye Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa uwezo wake wa kutembea juu ya mpira na kuwafurahisha kwa kuwapa burudani kwa wakati wote awapo uwanjani.

Ni kama utamaduni kwa mchezaji ambaye anawafunga watani anajitengenezea ufalme mkubwa kwenye timu hizo kongwe kwa kupendwa na mashabiki, sawa na alichokifanya Morrison kwenye mchezo uliopita ambao kimsingi Simba alionekana kupewa nafasi kubwa ya kushinda kutokana na ubora wa kikosi chao.

Yanga kupitia Morrison waliweza kutibua mipango ya wekundu hao kwa kupachika bao kwa mkwaju mkali wa adhabu uliopatikana baada ya nyota huyo kuangushwa nje kidogo ya eneo la hatari na kiungo wa Simba, Jonas Mkude.

Morrison alifanikiwa kutumia udhaifu wa safu ya ulinzi ya Simba na kuachia kiki iliyoenda kujaa moja kwa moja kwenye nyavu na kumuacha kipa Aish Manula akishangaa mashabiki wa upande wa pili wakishangilia kwa shangwe.

ANACHOKISEMA

Akizungumza na gazeti hili anasema kinachomfanya kuisumbua Yanga kwenye kipindi hiki sio kwamba yeye ni bora kuliko timu, bali amepata ofa kubwa kutoka klabu nyingine tofauti na aliyopewa na wanajangwani hao.

Anasema anafahamu majukumu yake na kazi ya mpira ni ya muda hivyo inapojitokeza ofa kubwa na timu inaonesha kuhitaji huduma yake analinganisha na kufanya maamuzi ambayo kwa sasa anauomba uongozi wa timu hiyo kukubali kuvunja mkataba naye.

“Nimepata ofa kubwa kuliko niliyopewa kutoka kwenye timu yangu sasa nimelinganisha na kuona ni bora niende sehemu nitakayolipwa mshahara mkubwa kwakuwa kazi ya mpira ni ya muda mfupi, ”anasema Morrison.

MATUKIO YANAYOFANANA

Tukio kama hili kujitokeza ndani ya Yanga sio mara ya kwanza kwani kuna matukio mengi yalikuja katika taswira hiyo na mwisho wa siku wachezaji waliondoka na kwenda kuanza maisha kwenye timu zingine mpya.

BANO KAKOLANYA

Kwa msimu uliopita Kakolanya alikuwa anaitumikia Yanga na alijizolea umaarufu mkubwa tu, kwa mashabiki wa timu hiyo baada ya kuonesha umahiri wa kudaka kwenye mchezo wa watani wa jadi, lakini mwisho wa siku alianza kuonesha dalili za utovu wa nidhamu.

Mwisho wa siku Kakolanya ilifikia hatua hadi anakimbia kambini usiku, tatizo lililoanza kutengeneza uhasama na aliyekuwa kocha wa kikosi hicho, Mwinyi Zahera na kutangaza hamtaki na kuanza kuwatumia makipa wengine kwenye michezo ya ligi hiyo.

Aidha, baada ya hali hiyo kuendelea ilipofikia msimu wa dirisha kubwa mchezaji huyo alisajiliwa na watani zao wa jadi Simba ambako anaendelea kuitumikia timu hiyo kwenye nafasi ya kipa licha ya kuwa chaguo namba mbili akizidiwa na Aish Manula.

HARUNA NIYONZIMA

Ni miongoni mwa wachezaji waliojizolea umaarufu mkubwa ndani ya timu hiyo kutokana na kuwa na uwezo wa kuuchezea mpira wawapo uwanjani na kuwapa burudani mashabiki.

Pamoja na ufalme huo mchezaji huyo ambaye ni raia wa Rwanda alikuwa kinara wa kufanya matukio ya ut- ovu wa nidhamu hata ilifikia hatua alihamia upande wa pili kwa maana ya kwenda upande wa Simba ambako aliitumikia kwa misimu miwili kabla ya kurejea tena ya Yanga.

MRISHO NGASSA

Aliachana na timu hiyo kwa matatizo ya kidhamu ambapo alienda kujiunga na klabu ya Azam FC na kuitumikia kwa kipindi cha msimu mmoja na baadae kujinga na Simba kwa kipindi kama hicho kabla ya kurejea Yanga kwa mara nyingine.

BAADA ya Namungo FC ...

foto
Mwandishi: Tuzo Mapunda

Post your comments

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi