loader
Dstv Habarileo  Mobile
Picha

Eymael hana wasiwasi na kikosi chake

KOCHA wa Yanga, Luc Eymael amesema kukosekana kwa Lamine Moro, Papy Tshishimbi na Bernard Morrison kwenye kikosi chake sio tatizo, kwani kuna wachezaji wanaoweza kuziba nafasi zao na kupata ushindi.

Wachezaji hao wanatarajiwa kuukosa mchezo huo dhidi ya Ndanda kwa sababu mbalimbali, ambapo Tshishimbi anasumbuliwa na matatizo ya kiafya wakati Moro na Morrison wanatumikia adhabu za utovu wa nidhamu baada ya kuadhibiwa na Shirikisho la Soka Tanzania (TFF).

Akizungumza Dar es Salaam, Eymael alisema kukosekana kwa wachezaji hao kuelekea kwenye mchezo dhidi ya Ndanda unaofanyika leo sio tatizo, kwani kikosi chake ni kipana chenye wachezaji wengi.

“Kukosekana kwa wachezaji Lamine Moro, Bernard Morrison na Papy Tshishimbi kikosi hakiwezi kuyumba kwani tuna kikosi kipana na wachezaji wa kuziba nafasi zao wapo, kikubwa tusubiri muda ufike,” alisema Eymael.

Alisema timu yoyote haiwezi kumtegemea mchezaji mmoja ndio maana kunakuwa na wachezaji wanaoweza kukaa kwenye vikosi vitatu ili kama mmoja akipatwa na tatizo, basi wanaosalia wanatakiwa kuziba nafasi pango.

Alisema malengo ya timu hiyo ni kushika nafasi ya pili na kwa kuwa bado kuna ushindani mkali, hawana budi kuendelea kushindana hadi dakika ya mwisho ili kutimiza lengo lao na kuwapa burudani mashabiki na wapenzi wa timu hiyo.

Yanga kwa sasa inashika nafasi ya tatu kwenye msimamo wa ligi hiyo wakiwa na jumla ya pointi 57 walizovuna baada ya kucheza michezo 31 na wanasaliwa na mechi saba anazotakiwa kupigania ili kumshusha Azam FC wanaoshika nafasi ya pili kwa pointi 58 wakiwa wamecheza mechi sawa.

BAADA ya Namungo FC ...

foto
Mwandishi: Mwandishi Wetu

Post your comments

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi