loader
Dstv Habarileo  Mobile
Picha

RC ataka bendi Arusha zishirikiane

MKUU wa mkoa Arusha, Iddi Kimanta amezitaka bendi za muziki wa dansi mkoani Arusha kuwa na ushirikiano ili kukuza sanaa hiyo na kuifikisha panapo stahili.

Akizungumza katika uzinduzi wa band mpya ya Wisdom Musica, Kimanta aliyekuwa mgeni rasmi katika hafla hiyo alisema vikundi hivyo vya sanaa vinasaidia kutoa ajira kwa wananchi, na hadi sasa mkoa wa Arusha una vikundi vingi vya band.

"Kuna watu wanaweza kuwa na mitazamo potofu kwamba kuwepo kwa bendi nyingine ni kupambana na zingine zilizo katika mkoa, lakini lengo sio hilo bali tunalenga Arusha ijitosheleze kwa kila kitu na nikiwa kama mkuu wa mkoa sitapenda au kusikia maneno ya uchonganishi wa aina hiyo, "alisema Kimanta.

Aliwataka wamiliki wa bendi lazima kujenge tabia za kupendana na kuaminiana kwani hata kama wanachukua wanamuziki bali wachukue kutoka mikoa mingine wa hapa wawaache hapo ili kujenga ushindani na Arusha kuwa miongoni mwa mikoa itakayokuwa bora kwenye dansi.

"Nimependezwa na wanamuzi Nyoshi, Mwinjuma na Bushoke kufika kuwaunga mkono Wisdom kitendo hicho kinaonesha ukomavu na wanafurahia mafanikio ya wanamuziki wenzao.

Alisema suala la sanaa na utamaduni ni miongoni mwa sera, ambazo wao kama viongozi wanatakiwa kuzitekeleza kwa sababu ni mojawapo ya utekeleza wa ilani ya Chama cha Mapinduzi.

Kwa upande wake mwanamuziki Nyoshi El Saadat 'Sauti ya Simba' alisema kila mmoja afanye bidii, kwani ni bendi, ambayo imejipanga vizuri na wakiendelea hivyo huko mbele watafika mbali.

"Nawasihi vijana hawa wasiwe na tamaa kama wana mapenzi ya bendi wawe pia na uvumilivu ili waweze kufika pale wanapopatarajia katika dansi waepuke lisambaratika na waache unafiki wasisahau kuzingatia nidhamu, “ alisema El Saadat.

Meneja wa Wisdom Musica, Cletus Wilbert alisema wanashukuru uzinduzi ulikwenda vyema na lengo ni kuifanya Arusha kuwa kubwa katika muziki wa dansi na sasa tutaanza kuzunguka nchi nzima,"alisema Wilbert.

Wasanii walionogesha uzinduzi huo ni Nyoshi El Saadat, Muumin Mwinjuma, Bushoke pamoja bendi mbalimbali zilisindikiza usiku huo wa Wisdom.

MWANARIADHA chipukizi wa kimataifa wa Tanzania, Regina Mpigachai, amepata ofa ...

foto
Mwandishi: Yasinta Amos, Arusha

Post your comments

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi