loader
Dstv Habarileo  Mobile
Picha

Wachezaji Gwambina wapongezwa

KOCHA Mkuu wa timu ya Gwambina FC, Fulgence Novatus amewapongeza wachezaji wake baada ya timu hiyo kupanda Ligi Kuu Tanzania Bara msimu wa 2020/2021.

Gwambina FC imepanda daraja baada ya kuibuka na ushindi wa bao 1-0 dhidi ya Pamba SC katika mchezo wa Ligi Daraja la Kwanza (FDL) uliochezwa katika Uuwanja wa CCM Kirumba jijini Mwanza.

Bao pekee la mchezo huo, lilifungwa na Meschack Abraham katika dakika ya 93.

Akizungumza na gazeti hili baada ya ushindi huo, Novatus alisema haikuwa safari rahisi kupanda Ligi Kuu kutokana na ligi hiyo kuwa ngumu na yenye upinzani mkubwa.

‘’Nawashukuru sana wachezaji wangu, viongozi, wadau na mashabiki wa timu yetu kwa kujitoa muda wote kwa ajili ya kuisaidia na kuishangilia timu yetu katika michezo yetu yote,’’ alisema Novatus.

Akielezea kuhusu ushindi wao dhidi ya Pamba SC, alisema mchezo ulikuwa mzuri sana na wachezaji wake walicheza kwa kufuata maelekezo muda wote, jambo liliosaidia kupata ushindi.

Gwambina FC imebakiza mechi mbili dhidi ya Rhino Rangers na Mashujaa FC, ambapo michezo yote itachezwa katika Uwanja wa Gwambina Complex wilayani Misungwi.

Gwambina FC inaongoza Kundi B ikiwa na alama 44 baada ya michezo 20 iliyocheza.

Nahodha wa Gwambina FC, Jacob Massawe alisema anawashukuru mashabiki wao, viongozi pamoja na wachezaji wenzake kwa kujitoa na kuweza kuisaidia timu yao kupanda Ligi Kuu

MWIGIZAJI maarufu wa tamthilia ya Karma, Wema Sepetu amewaomba radhi ...

foto
Mwandishi: Alexander Sanga, Mwanza

Post your comments

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi