loader
Dstv Habarileo  Mobile
Picha

Tiketi za kielektroniki kwa daladala Dar muhimu

HATUA ya serikali kuamua Jiji la Dar es Salaam kuanzia Julai Mosi mwaka huu kutumia tiketi za kielektroniki katika usafiri wa umma ni nzuri kwani si tu kupata takwimu halisi za namna ya kuboresha usafi ri lakini pia itasaidia katika ukusanyaji wa kodi kwa serikali na pia wamiliki kujua uhalisia wa mapato yao.

Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Isack Kamwelwe amenukuriwa na gazeti hili akisema matumizi ya tiketi za kielektroniki kuanzia wiki ijayo Julai Mosi yatasaidia kutoa tathmini halisi ya usafiri huo.

Kamwelwe akasema kwa sasa hakuna takwimu rasmi inayoonesha idadi ya watu wanaosafiri kwa kutumia usafiri wa daladala katika Jiji la Dar es Salaam kwa mwezi au kwa mwaka, hivyo siyo rahisi kuwahamasisha wawekezaji kuwekeza kwenye usafiri huo bila kuwapa mahitaji halisi kitakwimu.

Waziri Kamwelwe ameongelea zaid juu ya uwekezaji kama eneo litakaloangaliwa laikini pia, uendeshaji wa mabasi utakuwa ni rahisi kwa wamiliki ambao baada ya kununua magari, hawawezi kujua mapato halisi zaidi ya kuegemea taarifa kutoka ama kwa kondakta au dereva kutegemea aliyekabidhiwa gari.

Kamwelwe anasema mwaka mmoja baada ya kuanza matumizi hayo ya tiketi za kielektroniki, maofisa mipango watatoa taarifa ambayo pamoja na mambo mengine itasaidia kujua ongezeko na idadi ya watu wanaosafiri kwa kutumia usafiri wa umma kwa mwezi na hatimaye kwa mwaka mzima.

Akasema hatua hiyo itawezesha kujua mahitaji na kuhamasisha wawekezaji kuwekeza kwenye usafiri wa umma.

Tunaamini, hatua hiyo itawewezesha wamiliki pia kujua kiasi halisi cha fedha zinazokusanywa kwa siku, hivyo kuwawezesha kuwalipa wafanyakazi kulingana na mapato halisi.

Ni kutokana na wengi wa wamiliki kutojua uhalisia wa mapato, kumekuwa na tatizo la mikataba kwa wafanyakazi wa daladala, kila upande ukilalamika juu ya kutotendewa haki.

Upande wa kondakta na dereva wamekuwa wakidai kiasi cha fedha wanachopangia na wamiliki wa magari kila siku ni kikubwa, hivyo kuwafanya warudi nyumbani na fedha kidogo, huku wamiliki nao wakiamini fedha zinazokusanywa ni nyingi, kiasi cha kuona wanaofaidika na gari ni kondakta na dereva kuliko mwenye gari. Kutokana na kutoaminiana, suala la mikataba limekuwa likipigwa danadana lakini biashara ikiendelea.

TANZANIA itakuwa na ugeni mkubwa wa ...

foto
Mwandishi: Mhariri

Post your comments

Tangazo

CRDB

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi