loader
Dstv Habarileo  Mobile
Picha

Shule binafsi zilipe watumishi mishahara

LEO shule zote za awali, msingi na sekondari zinafunguliwa baada ya kufungwa kwa takribani miezi mitatu kutokana na tishio la homakali ya mapafu inayosababishwa na virusi vya corona.

Kabla ya kufunguliwa kwa shule hizo, mwezi moja uliopita vyuo vikuu nchini vilifunguliwa baada ya wanachuo kukaa nyumbani kwa muda.

Kufunguliwa kwa shule ni furaha kwa walezi na wazazi kwa kuwa watoto wamekaa nyumbani muda mrefu hali iliyofanya kuzorota usomaji kwani sio wote walioweza kusoma kwa njia ya video.

Ingawa ni furaha kwa wazazi na wanafunzi, kwa upande mwingine ni maumivu kwa walimu wanaofundisha shule hizo kutokana na ukweli kuwa janga hilo limesababisha shule zao kutowalipa mishahara kwa kukosa fedha.

Jambo hilo linaweza kushusha kiasi kikubwa ari ya kufanya kazi kwa walimu hao kwani hali ya kawaida limewaumiza mioyo yao, wamiliki wa shule hizo wangeweza kuchukua hatua zozote za kuwasaidia wakati wa janga kuwathamini.

Ikumbukwe kuna wanafunzi wa madarasa ya mitihani ambayo ni darasa la nne, la saba, kidato cha pili pamoja na kidato cha nne wanaohitaji kusaidiwa na walimu wao katika kipindi hiki.

Wakati umefika wamiliki wa shule binafsi kunusuru watoto wanaorudi shule kwa kuteta na walimu wao kuwalipa stahiki badala ya kujihalalishia hali iliyosababishwa na corona.

Jambo la walimu wa shule binafsi lisichukuliwe kirahisi kwani limesababisha familia nyingi kutokuwa na maelewano pale ambapo kwa miezi hiyo mitatu baba ameshindwa kuisaidia.

Picha kamili itadhihirika leo katika shule hizo baada ya kufunguliwa kama walimu na watumishi wengine wa shule hizo wakiwemo wapishi, madereva, wafanya usafi watakuwa na ari ya kufanya kazi kwa moyo maeneo yao.

Ieleweke sio shule binafsi ambazo hazikulipa mishahara wafanyakazi wao, zipo zilizotumia njia mbalimbali na kuzungumza na watumishi wao kuwafanya wajisikie sehemu ya shule hiyo.

Shule nyingine ziliwadhamini watumishi wao ili wapate mikopo kipindi hicho wanakipitia lakini ambao hawakujali waliwaacha wakataabika. Leo ndio siku ya uhalisia katika shule hizo binafsi ambazo hazikuwa na mchango wowote kwa watumishi wao kipindi cha janga la corona.

Katika hili inahitajika busara kwani watumishi hao nao ni binadamu na wana majukumu pia. Wanafunzi wa shule wataathirika kwa kukosa masomo yao ama kufundishiwa kwa kasi ndogo baada ya kukaa nyumbani kwa muda mrefu.

Kama mtumishi hasa mwalimu akikosa furaha ni wazi wanafunzi wataathirika kimasomo na kiafya na shule nyingi leo kutawaka moto.

Sio hao tu hata madereva wa wanafunzi watakosa ari ya kazi jambo ambalo litasababish wachelewe kufika shuleni au kutokufika kabisa. Busara itumike, wamiliki wa shule wakae na watumishi wao na kuleta maelewano na kazi katika shule hizo ziendelee bila wasiwasi.

KATIKA miaka ya karibuni msimu wa mavuno kumekuwa na watu ...

foto
Mwandishi: Lucy Ngowi

Weka maoni yako

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi