loader
Dstv Habarileo  Mobile
Picha

Kabudi atangaza nia kugombea ubunge

WAZIRI wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Profesa Palamagamba Kabudi ametangaza nia ya kugombea ubunge katika Jimbo la Kilosa mkoani Morogoro.

Profesa Kabudi ni Mbunge wa kuteuliwa na sasa anataka kuwa Mbunge wa Jimbo.

Alitangaza nia hiyo wilayani Kilosa jana kwenye hafla ya uwekaji wa jiwe la msingi wa handaki lenye urefu wa kilometa 1.1 na jiwe la msingi la ujenzi wa barabara ya Rudewa-Kilosa yenye urefu wa kilometa 24 uliofanywa na Rais John Magufuli.

Profesa Kabudi aliawaambia wananchi wa Kilosa kuwa yeye ni mzawa wa Kilosa kwa kuwa wazazi wake asili yao ni wilayani humo.

Kauli hiyo ilimfanya ashangiliwe na wananchi hao ambao awali walimpinga Mbunge wao aliyemaliza muda wake, Mbaraka Bawaziri kwa kupiga kelele alipopewa nafasi ya kuzungumza.

“Na mimi mtoto wenu ikimpendeza Mungu, na nikipata kibali, sikatai kuwa mtumishi wenu,” alisema.

Awali aliwataka wananchi wa Kilosa kutambua kuwa reli ya SGR ni fursa ya kuirudisha Wilaya hiyo katika heshima yake ya zamani ya maendeleo.

Profesa Kabudi pia alimuomba Rais Magufuli aifikirie Kilosa kuhusu ujenzi wa reli ya Kilosa- Mikumi-Kidatu hadi Mlimba hivyo kusaidia kuiunganisha Kilosa na Bonde la Kilombero.

UJENZI wa vituo vikubwa vitano vya kujazia nishati ya gesi ...

foto
Mwandishi: Matern Kayera, Morogoro

Weka maoni yako

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi