loader
Dstv Habarileo  Mobile
Picha

CCM Z’bar yafunga pazia urais, mmoja ajitoa

WAKATI shughuli ya uchukuaji fomu za kuomba ridhaa ya kugombea nafasi ya urais wa Zanzibar kwa tiketi ya CCM ikiwa inakamilika leo, zaidi ya wanachama 24 wamerudisha fomu huku Hussein Ibrahim Makungu akijitoa kwa madai ya kutoa nafasi zaidi kwa wagombea wengine na kurahisisha mchakato huo.

Katibu wa Idara ya Oganaizesheni ya Chama Cha Mapinduzi Zanzibar, Galous Nyimbo aliwataja wanachama watano waliorudisha fomu jana kuwa ni Pereira Ame Silima, Hasna Attai Masoud, Mussa Aboud Jumbe, Mmanga Mjengo Mjawiri na Ayoub Mohamed Mahmoud.

Makungu ambaye ni Mwakilishi wa Jimbo la Mtoni ametangaza kujiondoa katika kinyanganyiro cha wanachama wanaoomba ridhaa ya kupeperusha bendera ya CCM katika Uchaguzi Mkuu ujao kwa madai ya kutoa nafasi kwa wagombea wengine wenye uwezo kutetea nafasi hiyo.

“Nimekamilisha zoezi la kutafuta wadhamini wa mikoa mitano ya Unguja na Pemba, lakini nimeamua kujitoa ili niwapishe wanachama wengine wenye uwezo waendelee na kurahisisha mchakato huo,” alisema Makungu.

CCM ilitangaza kuwa kuanzia Juni 15, mwaka huu hadi leo saa 10:00 kamili jioni, itakuwa ni shughuli ya kuchukua na kurejesha fomu kwa ajili ya kuwania uteuzi wa chama hicho kuwa mgombea urais wa Zanzibar katika Uchaguzi Mkuu wa Oktoba, ambao Dk Ali Mohamed Shein atakuwa anamaliza muhula wake wa pili kikatiba.

NAIBU Waziri wa Kilimo, Omary Mgumba amesema Serikali imetekeleza miradi ...

foto
Mwandishi: Khatib Suleiman, Zanzibar

Weka maoni yako

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi