loader
Dstv Habarileo  Mobile
Picha

Viongozi vyama vya siasa waagizwa kujitathmini

SERIKALI imesema baadhi ya vyama vya siasa havina sifa nzuri katika matumizi ya fedha na mali za wanachama, jambo linaloathiri mwelekeo katika kujenga demokrasia.

Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge, Kazi, Ajira, Vijana na Watu wenye Ulemavu), Jenista Mhagama alisema hayo Dar es Salaam jana, na kutaka pia viongozi na vyama kujitathimini uzalendo wao, maadili na vinavyoimarisha amani na utulivu wa nchi.

Alikuwa akifungua kikao cha Msajili wa Vyama vya Siasa na viongozi wa kitaifa wa vyama hivyo 19. Kilihusu uhakiki wa vyama vya siasa na ripoti ya Mkaguzi na Mdhibiti Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG).

“Baadhi ya vyama vyetu havina sifa nzuri katika matumizi ya fedha na mali za chama. Hili jambo limekuwa likipigiwa kelele ama na wanachama au ripoti ya CAG. Baadhi ya vyama na viongozi wakuu wa vyama wanatumia vibaya mali na raslimali za wanachama,” alisema Jenista.

Alisema, “Sisi tunaojenga taswira ya kitaifa ni lazima tuhame uongozi tuliozoea tubadilike. Nashukuru Rais (John Magufuli) ameingia kupambana na ubadhirifu huo ndiyo mwelekeo. Tuombe viongozi wa vyama ubadhirifu siyo mwelekeo wa demokrasia na kujenga taasisi imara.”

Alisema rasilimali za vyama ni kwa ajili ya wanachama na Watanzania kwa ujumla na si kwa ajili ya viongozi wa vyama na kikundi kidogo cha watu.

Katika ripoti ya CAG ya mwaka 2018/2019, vyama vya siasa 12 kati ya 19 vyenye usajili wa kudumu, vilipata hati mbaya.

Kuhusu amani na utulivu, alisema pamoja na kuwapo tofauti za kiitikadi na kimtazamo, amani inapaswa kulindwa kwa nguvu.

Alisema amani ikipotea hakuna chama kitakachoweza kusimama.

“Kila chama na kiongozi ajue ana wajibu mkubwa wa chama chake, yeye binafsi, wanachama wenzake na viongozi wenzake, wanakuwa chachu ya kulinda amani, umoja, mshikamano na utulivu wa taifa letu,” alisema Jenista.

Alisisitiza, “Tunao washabiki wenye mihemuko, tunao baadhi ya viongozi ambao wako nyuma yetu wenye mihemuko, sisi kama viongozi wa kitaifa wajibu wetu ni kuhakikisha tunafanya taifa letu linaendelea hivi lilivyo kwa maana kwamba ni kisiwa cha utulivu ndani na nje ya bara.”

Alisisitiza vyama kushindana kwa hoja badala ya matusi, kejeli na ngumi na kutaka viingie kwenye uchaguzi vikiwa pamoja na kumaliza pamoja.

Aliwataka viongozi kuongoza kwa misingi ya kujali na kuzingatia uzalendo kwa nchi akisisitiza linapokuja suala lenye maslahi kwa nchi, vyama vibaki kuwa kitu kimoja. Alisisitiza vyama kujijienga kwa taswira ya umoja na kuepuka ubaguzi wa dini, ukabila na ukanda.

TIMU za Simba, Yanga na Mtibwa Sugar jana jioni zilijikuta ...

foto
Mwandishi: Stella Nyemenohi

Weka maoni yako

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi