loader
Dstv Habarileo  Mobile
Picha

Chadema yatoa mwongozo uchukuaji fomu

CHAMA cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), kimetoa utaratibu na ratiba kuhusu mchakato wa kugombea nafasi mbalimbali ikiwemo ya urais, ubunge na udiwani.

Mkurugenzi wa Uchaguzi Chadema, Reginald Munisi alitoa utaratibu huo baada Kamati Kuu kukutana Juni 26, mwaka huu na kujadili maandalizi ya chama kuelekea Uchaguzi Mkuu unaotarajiwa kufanyika Oktoba.

Alisema Kamati Kuu itamtaka mgombea urais ndani ya chama kuchukua fomu katika ofisi za Makao Makuu ya chama hicho kuanzia Julai 4, mwaka huu.

Munisi alisema kila mgombea urais atatakiwa kudhaminiwa na wanachama angalau 100 kwa kila kanda kwa zote 10 zilizopo.

“Mgombea ama wakala wake atatakiwa kuwasilisha fomu za kuomba uteuzi pamoja na viambatanisho vyote vilivyotajwa katika fomu na stakabadhi ya malipo ya fomu kwa katibu mkuu si zaidi ya Julai 19, mwaka huu saa 10 kamili jioni,” alisema Munisi.

Kuhusu mchakato wa urais, Katibu Mkuu atawasilisha taarifa kwa Kamati Kuu Julai 22 kisha kupendekeza jina au majina ya wagombea kwenda Baraza Kuu na Mkutano Mkuu kwa ajili ya mapendekezo ya uteuzi wa mwisho.

“Hakutakuwa na utaratibu wa kutia nia kwa mgombea mwenza. Fomu za urais itakuwa ni shilingi milioni moja,” alifafanua Mkurugenzi wa Uchaguzi Chadema.

Akizungumzia nafasi ya ubunge, alisema wagombea wote watatakiwa kujaza fomu za kuomba uteuzi wa kugombea nafsi hiyo ndani ya chama, na kwamba ratiba ya kuchukua, kujaza na kurejesha fomu za kugombea nafasi ya ubunge itaanza Julai 4 hadi Julai 10, mwaka huu.

Alisema fomu hizo zitatolewa na Ofisi ya Kanda za Chadema katika kanda zote 10 Tanzania Bara na Visiwani.

“Ratiba ya kura za maoni za Kamati za Utendaji za Chama (Jimbo), chini ya usimamizi wa kanda, zitaanza Julai 13 hadi Julai 17, mwaka huu,” alisema na kuongeza kuwa Kamati Kuu itafanya uteuzi wa wagombea wa nafasi ya ubunge Julai 30 hadi 31, mwaka huu.

WAZIRI wa Elimu, Sayansi na Teknolojia, Profesa Joyce Ndalichako amezipa ...

foto
Mwandishi: Lucy Ngowi

Weka maoni yako

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi