loader
Dstv Habarileo  Mobile
Picha

Asante JPM kwa New Mv Victoria

JUZI meli iliyokarabatiwa ya New Mv Victoria ‘Hapa Kazi Tu’ ilifanya majaribio ya safari katika Ziwa Victoria kati ya Jiji la Mwanza na Mji wa Bukoba, mkoani Kagera.

Meli hiyo yenye uwezo wa kutembea saa sita kutoka Mwanza hadi Bukoba, iliwasili Bukoba juzi saa 10 jioni, ikiwa na abiria kadhaa, akiwamo Katibu wa Itikadi na Uenezi wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Humphrey Polepole.

Polepole aliongoza kundi la viongozi 211 katika safari hiyo ya kwanza ya meli hiyo na kupokewa na maelfu ya wananchi wa mji huo na vitongoji vyake wakiongozwa na Mkuu wa Mkoa wa Kagera, Marco Gaguti.

New Mv Victoria inarejea kufanya safari zake katika Bandari za Mwanza na Bukoba tangu kusitisha safari hizo mwaka 2014.

Ujenzi wa meli hiyo unatokana na uamuzi wa Serikali ya Awamu ya Tano inayoongozwa na Rais John Magufuli, kutenga zaidi ya Sh bilioni 100 za mapato ya ndani kuunda meli mpya na kukarabati za zamani, kwa ajili kuwaondolea adha ya usafiri wananchi katika Ziwa Victoria.

Meli ya New Victoria ‘Hapa Kazi Tu’ ambayo ni utekelezeji wa ahadi ya Rais Magufuli aliyoitoa Bukoba wakati akiomba kura katika kampeni za Uchaguzi Mkuu wa mwaka 2015, imekarabatiwa kwa gharama ya Sh bilioni 22.7, ina uwezo wa kubeba abiria 1,200 na tani 200 za mizigo.

Uzinduzi wa meli hiyo, umekuwa faraja kubwa kwa wananchi wa mikoa ya Kanda ya Ziwa hasa Mwanza na Kagera, ambao kwa muda mrefu wamekuwa wakikabiliwa na adha kubwa ya kukosa usafiri wa uhakika na salama katika ziwa hilo.

Meli hiyo ni miongoni mwa mikakati lukuki ya serikali ya awamu ya tano kuboresha usafiri wa majini katika Ziwa Victoria, ambapo Aprili, mwakani, meli nyingine mpya ya Maziwa Makuu ambayo itafanya safari zake Afrika Mashariki katika bandari ya Bukoba, Mwanza, Kisumu na Bandari ya Uganda itazinduliwa mkoani Kagera.

Tunampongeza Jemedari Rais Magufuli kwa jitihada kubwa anazofanya usiku na mchana kuhakikisha kero mbambali zinazowakabili wananchi sekta za miundombinu, afya, elimu, maji na nyinginezo zinamalizika ili waweze kuishi maisha mazuri.

Rai yetu kwa wananchi wa Kanda ya Ziwa hasa wa mikoa ya Mwanza na Kagera, ni kuitunza meli hiyo ili iweze kudumu kwa muda mrefu, kwani ni mkombozi mkubwa kwao.

TANZANIA itakuwa na ugeni mkubwa wa ...

foto
Mwandishi: Mhariri

Post your comments

Tangazo

CRDB

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi