loader
Dstv Habarileo  Mobile
Picha

Wafanyabiashara waomba kupunguziwa gharama

WAFANYABIASHARA zaidi ya 100 wa matunda katika soko la Sabasaba jijini Dodoma wamemwomba Mkuu wa Mkoa Dk Bilinith Mahenge kuangalia suala la ushushaji wa mizigo ili kuwapunguzia gharama ambapo sasa mizigo yote inatakiwa kushukia soko jipya la Job Ndugai.

Walisema hayo jana wakati wa mkutano wao uliohudhuriwa na Ofisa Masoko wa Jiji la Dodoma, James Yuna. Michael Ngoi alisema wamekuwa wakiingia gharama kubwa kusafirisha mikungu ya ndizi.

“Kulitolewa tangazo kuwa magari yote makubwa na madogo yashushie mizigo 88 kwenye sojo jipya, jambo hili linatugharimu, tunawaza baada ya miezi mitatu mitaji itakuwa imekata kabisa,’’ alisema.

Alisema awali kabla ya agizo hilo mizigo ilikuwa ikishushiwa viwanja vya barafu na gharama ya kusafirisha mkungu sokoni ilikuwa Sh 700 lakini sasa gharama kusafirisha mkungu wa ndizi ni sh 2,600.

“Mzigo ukishukia soko jipya ukitaka kuupeleka soko la Sabasaba gharama ni kubwa, kushusha kila mkungu ni Sh 200, kubeba Sh 200, kupakia Sh 1,500, ukifika sokoni kushusha na kupeleka ndani ni sh 400 na hiyo ni gharama ya mkungu moja tu wa ndizi.

Mfanyabiashara mwingine, Matanza Matanza alisema waliwahi kupeleka malalamiko kwa mkuu wa mkoa lakini mpaka sasa hawajajibiwa. Ofisa Masoko wa Jiji la Dodoma, James Yuna alisema suala la kushusha mizigo soko la Ndugai lilitolewa na Mkuu wa mkoa, Dk Mahenge.

“Pale mfanyabiashara anapokuwa na hoja anasikilizwa, mkuu wa mkoa wakati anasema hayo alikuwa na nia njema tu, kuna wafanyabiashara soko jipya kwa hiyo mizigo ikishushwa pale wafanyabiashara wa pale wawe wananunua mizigo soko la jumla na kupanga kwenye vizimba vyao,” alisema.

Alisema hoja zao amezichukua na zitafikishwa mamlaka husika. “Hoja zenu nitazifikisha mamlaka husika na mtapatiwa majibu,” alisema.

foto
Mwandishi: Sifa Lubasi, Dodoma

Post your comments

Tangazo

CRDB

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi