loader
Dstv Habarileo  Mobile
Nchi EAC zisione aibu kuiga Tanzania

Nchi EAC zisione aibu kuiga Tanzania

MAAMBUKIZI ya virusi vya corona katika nchi za Jumuiya ya Afrika Mashariki yanaongezeka kila uchao.

Hata hivyo, nchini Tanzania mambo si mabaya kwani asilimia kubwa ya maambukizi ya virusi hivyo vinavyosababisha ugonjwa wa covid- 19 yamepungua kwa kiasi kikubwa kukaribia sifuri.

Hakuna miujiza iliyofanyika mpaka Tanzania kufikia hali hiyo, isipokuwa ni serikali kuchukua uamuzi wenye tija chini ya uongozi wa Rais John Magufuli kama mkuu wa nchi.

Uamuzi wa kiuongozi ni uamuzi uliojitosheleza usiohitaji maelekezo kutoka ndani au nje ya nchi. Tatizo la nchi nyingine za Afrika Mashariki zilicheza muziki ambao ngoma na ala zake zimetoka nje ya nchi hizo.

Hali imekuwa hivyo baada ya msimamo wa Jemadari wa Tanzania anayeamini katika kile anachokiamini na anachukua hatua katika kile anachokiamini.

Msimamo huo thabiti wa Rais John Magufuli ndio unatufanya kufurahia hali yetu na maisha mazuri ambayo hayajaathiriwa sana na virusi vya corona.

Hapa ndio tunapotoa ushauri kwa mataifa ya Jumuiya ya Afrika Mashariki kuiga mfano wa Tanzania.

Wasione aibu kwa sababu virusi vitawamaliza. Rais Magufuli alifanya nini mpaka Tanzania ikafikia hapa na kuwa mfano wa kuigwa Afrika na duniani kwa ujumla? Kiongozi huyo aliamini hofu inaua zaidi kuliko virusi hivyo.

Kwa ukweli huo, alichukua jukumu la kuwatoa hofu watu na kuuona ugonjwa wa Covid- 19 ni wa kawaida kama yalivyo magonjwa mengine.

Hii imewasaidia Watanzania kutopoteza maisha kiholela kwa kuwa hawana hofu wala woga wa kufa kutokana na corona.

Jambo la pili ambalo Rais Magufuli alifaulu ni kuhimiza Watanzania kufanya kazi kwa sababu aliamini virusi vya corona huwashambulia kirahisi watu wasiokula mlo kamili na wanaokaa na njaa muda mrefu.

Hivyo aliwahimiza Watanzania kufanya kazi muda wote huku wakichukua tahadhari dhidi ya maambukizi ya virusi hatari.

Wananchi waliitikia mwito wa Rais wao na kufanya kazi kwa bidii katika muda wote. Jambo la tatu ambalo rais wetu alifaulu kwa kiasi kikubwa ni kutofunga miji au nchi kwa kuwafungia watu wao ndani.

Hongera sana Rais Magufuli hapa ni kama ulioteshwa na Mwenyezi Mungu kuwa ungewatesa wananchi wako.

Hakika Rais Magufuli amefaulu kwa sababu kama angefunga mipaka na kuwafungia watu nje, uchumi wa wananchi ungesimama, wananchi wangekosa chakula, maji na matibabu, uchumi ungesimama na hali ingekuwa mbaya zaidi.

Mfano mzuri ni kwa majirani zetu, hali ni mbaya kila siku maambukizi yanapanda, walifungiana ndani hali ikawa mbaya zaidi, wakafunga mipaka ya nchi zao uchumi ukaanguka, kwa mujibu wa Benki ya Dunia.

Tunashauri majirani zetu wa Afrika Mashariki waige Rais Magufuli wananchi wao wale bata kama hapa Watanzania. Ukiangalia maambukizi katika nchi hizo ni hatari. Kenya ina maambukizi 5,533, Sudan Kusini 1,400, Uganda 933 na Rwanda 900 na maambukizi yanazidi kupanda kila siku.

https://apps.tsn.go.tz/public/uploads/76bc10a65558e0e85e308a8bd2ed5f93.jpg

LEO katika mwendelezo wa makala za ...

foto
Mwandishi: Selemani Nzaro

Post your comments

Tangazo

CRDB

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi