loader
Dstv Habarileo  Mobile
Picha

CAF, TFF waipongeza Simba

SHIRIKISHO la Soka Afrika (CAF) na Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) wameipongeza Simba kwa kutwaa mara tatu mfululizo taji la Ligi Kuu Tanzania Bara kwa msimu wa mwaka 2019/2020 na kukata tiketi ya kuiwakilisha nchi kwenye michuano ya kimataifa.

Pongezi hizo zinafuatia baada ya zile zilizotolewa awali na Kocha Mkuu wa Yanga, Luc Eymael aliyeipongeza Simba wakati ikielekea kucheza na Tanzania Prisons, mchezo ulioipa ubing-wa licha ya kutoka suluhu juzi kwenye Uwanja wa Kumbukumbu ya Sokoine, Mbeya.

Simba ilitangazwa bingwa baada ya kufikisha pointi 79, ambazo haziwezi kufikiwa na timu yoyote, hata Yanga ambayo sasa ina pointi 60, ambayo kama itashinda mechi zake sita zilizobaki, itaishia kufikisha pointi 78.

CAF, kupitia kwenye mtandao wake wa kijamii wa Twita imeipongeza Simba kwa kuwa mabaingwa wapya na kuwakaribisha katika mashindano ya kimataifa, tayari kwa kuiwakilisha nchi.

“Hongera kwa timu ya Simba kuwa mabingwa wapya wa Ligi Kuu Tanzania Bara,“ulisomeka ujumbe kwenye mtandano huo.

TFF, kupitia kwenye mitandao wake wa kijamii wa Instagramu na Twita umeipa Simba kongole kwa hatua hiyo na kuwatakia kila la heri na maandalizi mema ya maandalizi ya michuano ya kimataifa.

Pia Mwenyekiti wa zamani wa Simba Ismaili Rage amefurahia kwa Simba kubeba ubingwa, huku wakiwa na mechi sita mkononi wameonesha wao ni bora na anawatakiwa safari nje na kuliwakilisha vizuri nchi kimataifa.

Rage alisema utamaduni wa Simba siku zote ni kwenda kushiriki michuano ya kimataifa, ubingwa ni kitu kizuri kwakuwa wanapata fedha na kutengeneza historia kwa wachezaji.

“Simba tumechoka kila siku kushindana na Yanga, sisi ni lazima kuwa mabingwa kwakuwa Yanga na Simba tumeanza kushindana toka nchi haijazaliwa, sasa tunahitaji kufanya vizuri kimataifa ili tuwe mfano kwa timu zingine, “alisema Rage.

MWIGIZAJI maarufu wa tamthilia ya Karma, Wema Sepetu amewaomba radhi ...

foto
Mwandishi: Mwandishi Wetu

Post your comments

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi