loader
Dstv Habarileo  Mobile
Picha

Kocha akutwa na corona

KOCHA aliyeisaidia Argentina kutwaa taji la Dunia mwaka 1986, Carlos Bilardo amelazwa hospitalini baada ya kubainika kuwa na virusi vya corona, lakini hakuwa na dalili zozote, kwa mujibu wa vyombo vya habari vya hapa.

Familia yake imesema kuwa Bilardo amekuwa akitibiwa katika Taasisi ya Uchuguzi wa Magonjwa ya Argetina iliyopo katika jiji hilo.

Imeelezwa kuwa afya yake inaendelea vizuri, kwa mujibu wa ndugu zake. Kocha huyo mwenye umri wa miaka 82 alikuwa akisumbuliwa na afya ya akili na alikuwa akiishi katika makazi ya wagonjwa pamoja na watu wengine 10, ambao nao walikutwa na covid-19.

Anapata msaada kutoka Estudiantes La Plata, klabu yake ya zamani, ambayo aliichezea na baadaye kuifundisha.

"Tuko pamoja na wewe Carlos!" mtandao huo ulituma taarifa katika Twitter juzi. Bilardo Julai mwaka 2019 alilazwa katika chumba cha wagonjwa mahututi akisumbuliwa na shinikizo la damu.

Aliifundisha timu ya taifa ya Argentina kuanzia mwaka 1982 hadi 1990, akishinda Kombe la Dunia nchini Mexico akiwa pamoja na Diego Maradona na baadaye aliongoza timu hiyo kutetea taji hilo hadi kucheza fainali za mwaka 1990 nchini Italia.

Pia ni daktari. Argentina imerekodi karibu vifo 1,200 na kesi zaidi ya 55,000 za virusi vya cora. Rais Alberto Fernandez alitangaza Ijumaa hatua ngumu za kuzuia watu kukaa ndani katika jiji la Buenos Aires na maeneo ya jirani, ambayo kesi za corona zimeongezeka.

MWIGIZAJI maarufu wa tamthilia ya Karma, Wema Sepetu amewaomba radhi ...

foto
Mwandishi: BUENOS AIRES, Argentina

Post your comments

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi