loader
Dstv Habarileo  Mobile
Wajumbe 9 wazazi CCM mbaroni

Wajumbe 9 wazazi CCM mbaroni

Taasisi ya Kuzuia na Kupamba na Rushwa (TAKUKURU) mkoani Arusha imewatia mbaroni wajumbe tisa wa Jumuiya ya Wazazi ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) kwa tuhuma ya kutoa rushwa.

Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa kwa vyombo vya habari jana na Kaimu Kamanda wa Takukuru, Mkoa wa Arusha, James Ruge, waliotiwa nguni ni pamoja na Sifael Pallangyo, Mjumbe wa Baraza la Jumuiya ya Wazazi Mkoa wa Arusha, Upendo Ndorosi, Katibu wa Walezi Wilaya ya Longido na Laraposho Laizer, Katibu wa Wazazi Wilaya ya Longido na Mjumbe wa Baraza la Wazazi, Mkoa wa Arusha.

Wengine waliotajwa katika taarifa hiyo ni Godwait Mungure, Katibu wa Wazazi Kata ya Kikatiti, Wilaya ya Meru, Mikidadi Mollel, Mwenyekiti wa Kamati ya Pembejeo Kijiji cha Tukusi, Kata ya Lolkisale Wilaya ya Monduli.

Wamo pia Kanankira Nnyary Wakala wa Pmbejeo za Kilimo, Kijiji cha Loita, Kata Nkonrua Halmashauri ya Meru, Gervas Mollel, mfanyabiashara Kata ya Oltumet Wilaya ya Arumeru na Joseph Mollel, mfanyabiashara wa kata hiyo.

Taarifa hiyo ilisema Juni 26 mwaka huu, Takukuru Mkoa wa Arusha ilipokea taarifa toka kwa raia mwema kwamba, Lilian Ntiro ambaye anatarajiwa kugombea ubunge kupitia Wazazi, Mkoa wa Arusha alimpatia Pallangyo fedha kwa ajili ya kwenda kuhonga wajumbe wa baraza la wazazi wilayani Longido kama kishawishi ili apigiwe kura katika kura za maoni ndani ya CCM zinazotarajiwa kupigwa mwezi ujao.

Baada ya kupokea taarifa hiyo ya raia mwema Takukuru Mkoa wa Arusha kwa kushirikiana na maofisa wa taasisi hiyo Wilaya ya Longido, waliandaa mtego na kufanikiwa kuwakamata watuhumiwa wanne kila mmoja akiwa na kiasi cha fedha zikiwa zimeandaliwa kwa ajili ya kuwahonga wajumbe wa baraza la wazazi Longido.

Taarifa hiyo ilisema kuwa Sifael Pallangyo alikamatwa na kiasi cha Sh 140,000 , Upendo Malulu alikamatwa na Sh 552,000 pamoja na simu ya Aitel iliyoonesha mawasiliano na watuhumiwa wenzake.

Kwa mujibui wa taarifa hiyo, watuhumiwa wengine ni pamoja na Laraposho Laizer aliyekutwa na Sh 117,000 pamoja na simu aina ya Sumsung Galaxy ambapo kulikuwa na mawasiliano na watuhumiwa wenzake. Mwingine ni Godwait Mungure aliyekutwa na simu ndogo ikiwa na mawasiliano na mtuhumiwa mwingine ambaye ni Sifael Pallangyo.

Takukuru Mkoa wa Arusha inawashukuru wananchi wa mkoa huo kwa ushirikiano na imewaomba kuendelea kutoa taarifa katika kipindi hiki cha kuelekea Uchaguzi Mkuu wa urais, ubunge na udiwani huku taasisi hiyo ikiahidi kuzifanyia kazi taarifa zao kwa haraka.

Pia Takukuru ilitumia taarifa hiyo kuwaonya wate walianza kuwarubuni wapiga kura kwa rushwa na kufanya kampeni kabla ya muda kwa kuwa vitendo hivyo ni kinyume na sheria za uchaguzi.

https://apps.tsn.go.tz/public/uploads/cea2aac8646d37a4fd3ab14a9835ef51.jpg

ALIYEKUWA Mbunge Mteule wa Jimbo la Konde ...

foto
Mwandishi: John Mhala, Arusha

Post your comments

Tangazo

CRDB

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi