loader
Dstv Habarileo  Mobile
Picha

Waziri awapa Tanesco siku 5

WAZIRI wa Nishati, Dk Medard Kalemani ametoa siku tano kwa Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO) kulipa fi dia kwa wananchi wa Kidahwe waliopisha ujenzi wa Kituo cha Kupoza Umeme cha Kidahwe katika Kijiji cha Kidahwe, Kata ya Kidahwe Wilaya ya Kigoma mkoani Kigoma.

Agizo hilo amelitoa mwishoni mwa wiki wakati akiwa kwenye uzinduzi wa hatua ya kuanza kuwalipa fidia zao, wananchi ambao wameridhia kutoa ardhi yao kwa ajili ya ujenzi wa kituo hicho cha kupoza umeme Kidahwe.

Dk Kalemani alisema zaidi ya Sh milioni 700 zipo tayari kwa malipo ya wananchi 411 na kuwataka Tanesco kuanza mara moja kuwalipa wananchi hao na kuwapa siku tano tu kumaliza kazi hiyo.

“Niliacha maelekezo kwa waatalamu wetu kufanya kazi mbili, kazi ya kwanza ilikuwa kuhakikisha wananchi wanaozunguka maeneo ya mradi ambao wanapitiwa mradi wafanyiwe tathimini na kulipwa fidia zao na jambo hili tayari limeanza kufanyiwa kazi na jambo la pili ni kuanza matayarisho ya ujenzi wa mradi mkubwa huu,” alisema.

Aliwashukuru wananchi wa eneo hilo kwa kutoa maeneo yao kwa ujenzi wa kituo hicho kikubwa chenye uwezo wa kuzalisha umeme wa kilovolti 400 ambao unatarajiwa kuondoa kero ya upatikanaji wa umeme mkoani humo. Aliwataka wananchi watakaolipwa fidia hiyo kuzitumia vizuri fedha zao vizuri kwa kununua maeneo mengine na kujiendeleza kiuchumi.

“Mtakaolipwa fedha zenu msije mkazitumia vibaya fedha hizo halafu mkarudi tena Tanesco kudai nyingine,” alisema.

Aliwataka Tanesco kuanzia Julai 5, mwaka huu waanze mara moja ujenzi wa kituo hicho ili wananchi wa Kigoma waanze kupata umeme wa uhakika ambao utawasaidia kujenga uchumi wao, wa mkoa na Taifa kwa jumla.

Mkuu wa Mkoa wa Kigoma, Emmanuel Maganga aliwashukuru wananchi wote waliotoa maeneo yao kwa ajili ya maendeleo ya mkoa huo na amewahakikishia fedha za malipo zipo tayari.

Pia aliwatahadharisha watakaolipwa fidia hawataruhusiwa kuyatumia tena maeneo hayo kwani ni mali ya serikali. Dk Kalemani pia ametembea Kituo cha Kupoza Umeme cha Nguruka Kijiji cha Mganza na kuwataka Tanesco kumaliza ujenzi wa kituo hicho Julai mwaka huu.

BENKI za NIC Tanzania na CBA ...

foto
Mwandishi: Mwandishi Maalumu, Kigoma

Weka maoni yako

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi