loader
Dstv Habarileo  Mobile
Picha

TMDA yazindua awamu ya 4 mkataba wa huduma

MAMLAKA ya Dawa na Vifaa Tiba (TMDA) imezindua awamu ya nne ya mkataba wa utoaji huduma kwa wateja kupunguza muda uliokuwa ukitumika kusajili dawa zinazotoka nje na maeneo ya biashara.

Akizungumza wakati wa uzinduzi wa mkataba huo, Mganga Mkuu wa Serikali, Profesa Abel Makubi, mbali na kuipongeza TMDA kwa hatua hiyo, pia alizitaka taasisi nyingine vikiwemo vituo vya afya kuhakikisha vinaiga mfano huo ili kuweka mazingira mazuri katika sekta ya afya.

Profesa Makubi alisema kuzinduliwa kwa mkataba huo ina maana kubwa katika utendaji wa taasisi hiyo na serikali kwa ujumla, hivyo ni vyama TMDA ikahakikisha inausimamia kikamilifu ili kuleta ufanisi hususani kwa watoa wa huduma na taasisi nyingine zinazohusika kwa karibu na mamlaka hiyo.

“Imani yangu ni kuwa mkataba huu utakapoanza kutumika rasmi kuanzia leo utatusaidia kutoa huduma bora kwa wateja wa ngazi zote mnaowahudumia na kuondoa changamoto zilizokuwa zikijitokeza awali,” alisema Profesa Makubi.

Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa TMDA, Adam Fimbo alisema kuzinduliwa kwa awamu hiyo ya nne ya mkataba kunatokana na mapitio ya mkataba wa wateja wa lugha ya kigeni na baada ya utekelezaji wa mkataba uliokuwa umeandaliwa mwaka 2016.

Alisema mapitio ya mkataba uliopita umechagizwa na mabadiliko mbali mbali yaliyojitokeza katika kipindi cha miaka minne iliyopita ikiwa imejumuisha majukumu yaliyokuwa chini ya iliyokuwa Mamlaka ya Chakula na Dawa (TFDA) ambayo baadhi ya majukumu yake yalihamishiwa Shirika la Viwango Tanzania (TBS).

Alisema awamu hiyo ya nne ya mkataba wa huduma kwa wateja kimsingi umezingatia mambo mbali mbali ikiwemo uwekaji wa mifumo ya Tehama, msukumo kukuza sekta ya viwanda ambako sera, miongozo na taratibu zake zimepitiwa kuvutia uwekezaji na uwekaji wa viwanda vya dawa na vifaa tiba.

Pamoja na hilo, majukumu mengine ya mkataba huo ni kuweka mikakati mbali mbali ya kuweka mazingira wezeshi ya kibiashara na kupunguza urasimu katika utoaji wa huduma na kusisitiza kuwa hatua hiyo ya kuzinduliwa kwake kutasaidia kuleta mabadiliko kwa kiasi kikubwa ndani ya sekta hiyo ya afya.

Alitolea mfano wa baadhi ya faida zitakazopatikana kupitia mkataba huo wa toleo la nne ni kupunguza muda wa usajili wa dawa kutoka siku 120 hadi siku 60, usajili wa maeno ya biashara za bidhaa zinazodhibitiwa na TMDA ukipungua kutoka siku 10 hadi 8.

Aidha, alisema pamoja na kupunguza siku za kutathmini na kusajili dawa, kupitia mkataba huo, TMDA imeweka utaratibu rahisi wa kusajili dawa zilizosajiliwa kupitia jumuiya za kikanda, Afrika Mashariki (EAC) na ya Maendeleo Kusini mwa Afrika (SADC) pamoja na Shirika la Afya Duniani (WHO).

WAZIRI wa Elimu, Sayansi na Teknolojia, Profesa Joyce Ndalichako amezipa ...

foto
Mwandishi: Oscar Job

Weka maoni yako

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi