loader
Dstv Habarileo  Mobile
Picha

Wanahisa DCB kupata neema

WANAHISA wa Benki ya Biashara ya DCB ya jijini Dar es Salaam wana kila sababu ya kuwa na matumaini makubwa na benki yao baada ya bodi ya benki hiyo kutangaza gawio la Sh 5.40 kwa kila hisa wakati wa Mkutano Mkuu wa Mwaka wa Wanahisa wa DCB uliofanyika jijini Dar es Salaam mwishoni mwa wiki.

Akitangaza gawio hilo lililopitishwa na wanahisa wote kwa njia ya mtandao, Mwenyekiti wa Bodi ya DCB anayemaliza muda wake, Profesa Lucian Msambichaka alisema gawio hilo limetokana na faida waliyopata ya Sh bilioni 2.038 baada ya kodi hadi Desemba 31, 2019 huku kiasi cha Sh milioni 500 kikitumika kulipia gawio hilo.

Alisema bodi iliamua kulipa gawio hilo licha ya faida waliyopata kwa kuzingatia sababu mbalimbali ikiwemo hali ya kibiashara iliyopo nchini iliyochangiwa kwa kiasi kikubwa na athari za ugonjwa wa homa kali ya mapafu, Covid-19.

“Sababu nyingine muhimu iliyochangia azma ya kutoa gawio hili ni kutumia faida hiyo kuiwezesha benki kuendelea kuimarisha mtaji hivyo kuendelea kufanya kazi kwa ufanisi na kupata faida.

“Mafanikio ya DCB yanachangiwa kwa kiasi kikubwa na mchango mkubwa unaotoka kwa wanahisa wa benki yetu kwani hata mwaka 2018 pale benki yetu ilipopata faida ya Sh milioni 995, bado wanahisa wetu waliazimia kutumia faida hiyo kuimarisha mtaji badala ya kugawana faida,” aliongeza Profesa Msambichaka.

Akizungumza na wanahisa hao, Mkurugenzi Mtendaji wa DCB, Godfrey Ndalahwa alisema benki imeendelea kuimarika kimtaji huku wakitimiza kwa uhakika maazimio yaliyofikiwa na mkutano mkuu wa wanahisa mwaka jana.

Alisema moja ya maazimio ya mkutano huo ilikuwa ni benki kutanua wigo wake na kuwa na mawakala jijini Dar es Salaam na mikoani huku azimio lingine likiwa ni kupunguza kiwango cha mikopo chechefu.

“Hayo tuliyachukua na sasa tuna mawakala nchi nzima na vituo vidogo vya kutolea huduma vitano na matawi manane huku tukifanya vizuri kupunguza mikopo chechefu kwa kuchukua hatua na kuimarisha kitengo cha ukusanyaji madeni na kudhibiti mawakala wanaokusanya madeni na kuweka utaratibu mzuri ili mikopo ikidhi taratibu,” alisema Ndalahwa.

“Matokeo ya hatua hizi ni kuwa tumepunguza mikopo chechefu kwa asilimia 19 mwaka 2018 hadi asilimia 14 mwaka 2019 na tumepunguza mikopo safi kwenda chechefu kutoka asilimia 2.6 hadi 0.3 mwaka 2019 na tunaendelea kuhakikisha kwamba mikopo inayotolewa inakuwa na uhakika wa kurejeshwa,” aliongeza.

Akizungumzia utendaji wa kifedha, Kaimu Mkurugenzi wa Idara ya Fedha ya DCB, Ester Bgoya alisema moja ya sababu benki kufanya vizuri ni kupungua kwa gharama za uendeshaji mwaka jana kutoka Sh bilioni 17 hadi bilioni 15.8 kutokana na udhibiti wa matumizi yasiyo ya lazima na kuboresha uendeshaji biashara kwa kutumia teknolojia.

“Pamoja na kuwa tumekuwa na ongezeko la mikopo mwaka 2019 mapato ya riba yanaonekana kushuka kutoka shs bilioni 15.7 hadi bilioni 12.5 kulikosobabishwa na kushuka kwa riba za mikopo ikiwa ni malengo ya benki kushusha na kutoa mikopo nafuu,” alisema Bgoya.

SERIKALI imesema nchi ina chakula cha kutosha, lakini kuna uwezekano ...

foto
Mwandishi: Mwandishi Wetu

Post your comments

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi