loader
Dstv Habarileo  Mobile
Picha

Magufuli- Msiumizane, msikibomoe chama

Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Dk John Magufuli amewataka wanachama wa chama hicho wanaotaka kugombea nafasi za uongozi wakati wa Uchaguzi Mkuu mwaka huu waepuke siasa zitakazokibomoa chama hicho.

Dk Magufuli amewataka wagombea hao wakiwemo wa ubunge, uwakilishi na udiwani wafanye kampeni kistaarabu kwa kutanguliza maslahi ya chama na Tanzania.

Amewataka wana- CCM wazitumie kampeni kukibomoa chama hicho na kusababisha wawe wameumia wakati wa uchaguzi.

“Niwaombe sana wana- CCM tukawe wavumilivu, tukawe wavumilivu, kwa sababu nimeanza kuiona hiyo dalili hata kwa wagombea ishirini na kitu kule Zanzibar…wengine wanatumia mtandao wanamsema mwenzao, wengine kwenye magazeti lakini atakayechaguliwa ni mmoja tu, atakayechaguliwa ni mmoja tu na Mungu wetu wa mbinguni anamfahamu”amesema jijini Dodoma.

Ametoa angalizo hilo leo baada ya kurudisha fomu alizochukua Juni 17 mwaka huu kuomba chama hicho kimpitishe awe mgombea wa urais wa Tanzania wakati wa uchaguzi huo unaotarajiwa kufanyika Oktoba mwaka huu.

Hadi mchana wa leo kiongozi huyo alikuwa mwana- CCM pekee aliyechukua fomu kuomba CCM impitishe awe mgombea urais.

Kwa mujibu wa Dk Magufuli, ameomba tena CCM imteue agombee urais ili akichaguliwa akamilishe mipango mingi ambayo tayari imeanza kutekelezwa wakati wa kipindi cha kwanza cha Serikali ya Awamu ya Tano.

“Bado tuna changamoto nyingi katika taifa letu…mipango mingi sana tumeitekeleza, hata ile ambayo haikupangwa tumeitekeleza lakini napenda nikiri ndugu zangu kwenu wakati mimi na ninyi tukitekeleza mipango hii tumegundua kuna mipango mingi zaidi inatakiwa kutekelezwa…na siamini kama atatokea mwingine wa kuikamilisha vizuri kama sisi tuliyoianza”amesema.

Zaidi ya wanachama milioni moja wa CCM wamemdhamini kiongozi huyo ili chama hicho kimpitishe agombee urais wa Tanzania.

“Kwangu mimi hili ni deni kubwa, ni deni kubwa kwa Watanzania, ni deni kubwa kwa wana- CCM”amesema nje ya ofisi za CCM maarufu kwa jina la White House.

Rais John Magufuli amemteua Dk Philemon Sengati kuwa Mkuu wa ...

foto
Mwandishi: Basil Msongo

Weka maoni yako

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi