loader
Dstv Habarileo  Mobile
Picha

Milioni 500/- zatolewa ujenzi hospitali Sumbawanga

MKUU wa Mkoa wa Rukwa, Joachim Wangabo amesema Sh milioni 500 zimetolewa na serikali kwa ujenzi wa hospitali ya wilaya Manispaa ya Sumbawanga, akiagiza ujenzi wa majengo ya kutolea huduma kwa wagonjwa wa nje na mama na mtoto yakamilike na kufanya kazi ifikapo Oktoba mwaka huu.

Hospitali hiyo inajengwa Isofu ambalo liko umbali wa kilometa saba kutoka Sumbawanga Mjini.

“Tayari viwanda 300 vimepimwa kuzunguka eneo hilo ambalo inajengwa hospitali hiyo pia barabara ya kufika katika eneo hiyo inatengenezwa,” alisema Wangabo.

“Hospitali za wilaya za Kalambo, Nkasi na Sumbawanga inayojengwa Bonde la Ziwa Rukwa Kijiji cha Mtowisa Halmashauri ya Sumbawanga zinatoa huduma ya afya ya mama na mtoto pia wagonjwa wa nje. Hivyo naagiza na hii inayojengwa Isofu ianze kutoa huduma hizo ifikapo Oktoba mwaka huu,” alieleza.

Alibainisha hayo juzi wakati wa hafla ya kukabidhi hundi kwa vikundi 14 vya wafu wenye ulemavu na Chama cha Akiba na Mikopo cha Vijana ya New Bodaboda Saccos ambavyo kwa pamoja wamekopeshwa na Manispaa ya Sumbawanga mikopo yenye thamani ya Sh 110,662,500.

Pia aliwakabidhi pikipiki 35 kwa New Bodaboda Saccos zenye thamani ya Sh 78,662,500. Mkurugenzi wa Manispaa ya Sumbawanga, Jacob Mtalitinya alisema imetoa mikopo isiyo na riba kwa vikundi vya vijana, watu wenye ulemavu, wanawake na Saccos ya Sh 488,340,500 kwa miaka miwili mfululizo ya fedha 2019/20.

Utoaji wa mikopo hiyo ya uwezeshaji wananchi kiuchumi ni agizo la serikali kupitia Wizara ya Ofisi ya Rais-Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (Tamisemi) la utoaji wa asilimia 10 la pato la makusanyo ya ndani kwa vijana, wanawake na watu wenye ulemavu.

Akifafanua alisema katika robo ya nne ya mwaka wa fedha 2019/20, Manispaa ya Sumbawanga imefanya tathmini kupitia kamati yake ya utoaji mikopo isiyo na riba kwa vikundi 14 na Saccos moja ya vijana ya New Bodaboda na kubaini vyote vinavyohitajika sifa ya kukopeshwa.

Alisema katika mwaka wa fedha uliomalizika, vikundi 55 na Saccos moja ya vijana yenye wanufaika 378 wamekopeshwa mikopo isiyo na riba yenye thamani ya Sh 235,112,500 ikiwa ni sawa ya asilimia 102 ya lengo la kutoa mikopo yenye thamani ya Sh 231,251,000 kulingana na makusanyo ya kibajeti.

Mwenyekiti wa Waendesha Bodaboda Manispaa ya Sumbawanga, Leonard Mirambo alisema watahakikisha wanarejesha mkopo wa pikipiki kwa wakati, na pia wataendelea kutoa huduma za usafiri wa bodaboda katika manispaa hiyo kwa kuzingatia sheria za usalama barabarani

JESHI la Polisi kupitia Kikosi cha Farasi, limeanzisha huduma ya ...

foto
Mwandishi: Peti Siyame, Sumbawanga

Weka maoni yako

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi