loader
Dstv Habarileo  Mobile
Picha

CCM yaonya kuhusu wagombea mifukoni

WANACHAMA wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Mkoa wa Arusha wamesisitizwa kuacha kuwa na wagombea mifukoni ilhali chama hakijaanza kugawa fomu kwa ajili ya udiwani na ubunge.

Aidha, wamesisitizwa kuacha tabia ya kuwa wasemaji kwenye makundi mbali mbali ya kijamii kwani chama kina wasemaji kuanzia ngazi ya kata hadi mkoa. Rai hiyo imetolewa na Mwenyekiti wa Jumuiya ya Wazazi CCM Wilaya ya Arusha Mjini, Ally Meku wakati alipokuwa akizungumza na wanachama wa CCM Kata ya Sinoni jijini Arusha.

Meku alisema katika uchaguzi baadhi ya wanaCCM wanakuwa na wagombea wao na makundi lakini hayasaidii chama kwani mgombea atakayepitishwa na CCM ndiye atakuwa mgombea ubunge wa wote. Alisema kama kuna kiongozi wa CCM anafanya uovu kata mbali mbali kwa kuhonga wanachama, basi watoe taarifa ngazi husika.

“Acheni kusema eti kada mtiifu, bali semeni majina yenu na sisi viongozi hatutawataja huko mbele ya safari bali tutachukua hatua kwa mtu aliyesababisha maovu,” alisema Meku.

Mwenyekiti wa CCM Kata ya Sinoni, Ally Mrimbo alisema kila mwanaCCM ni imara kuhakikisha maendeleo ya kila maeneo yanakuwepo ikiwemo kutotenganishwa na watia nia kwa rushwa na kusisitiza hatakubali kuona wanachama wanasambaratishwa sababu ya rushwa kwa kupewa fedha na watia nia.

Rais John Magufuli amemteua Dk Philemon Sengati kuwa Mkuu wa ...

foto
Mwandishi: Veronica Mheta, Arusha

Weka maoni yako

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi