loader
Dstv Habarileo  Mobile
Picha

Asasi 245 kutoa elimu ya mpiga kura, 97 uangalizi

TUME ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) imetoa vibali kwa asasi za kiraia 245 kutoa elimu ya mpiga kura huku nyingine 97 zikipatiwa vibali vya kufanya shughuli za uangalizi wa Uchaguzi Mkuu utakaofanyika Oktoba mwaka huu.

Mkurugenzi wa Uchaguzi wa NEC, Dk Wilson Charles alibainisha hayo jana na kuongeza kuwa asasi hizo zote zinapaswa kuwasilisha NEC ratiba nzima inayoonesha lini na wapo kazi yao hiyo itaanza.

Alisema pia asasi hizo zinapaswa kuwasilisha katika ofisi za NEC orodha ya majina ya wafanyakazi wao watakaoshiriki katika kazi hizo za tume huku pia wakitakiwa kuelezea kuhusu vyao vya fedha za kazi hizo.

Alisema NEC ilipokea maombi mengi, isipokuwa asasi hizo tu ilizozitaja ndio zimekidhi vigezo wakati zilizoachwa zilibainika kuwa na makosa mbalimbali. Alitaja kati ya sababu ni asasi kushindwa kuwa na ofisi ya kufanyia kazi kasoro ambazo alibainisha kuwa zilitokea katika asasi nyingi.

Kasoro nyingine alibainisha kuwa ni baadhi ya asasi kuomba fursa ya kutoa elimu ya uraia wakati NEC ilitaka asasi ambazo zinaweza kutoa elimu ya mpiga kura wakati wa uchaguzi mkuu.

Pia alisema asasi nyingine zilishindwa kutoa taarifa zake kuhusu matumizi ya fedha zake ikiwa na maana ya kuwa hazikuwa zimekaguliwa na nyingine kushindwa kabisa hata kuonesha ni kwa kiasi gani zimetimiza malengo yake.

Alibainisha kuwa baadhi ya asasi zilijichanganya katika kufanyiwa usajili wake ambapo nyingine badala ya kusajiliwa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi zimesajiliwa kwa Wakala wa Usajili wa Biashara na Leseni (BRELA).

Kujichanganya huko pia kulihusisha asasi kusajiliwa kwa Wakala Wa Usajili, Ufilisi na Udhamini (RITA) wakati zikipaswa kusajiliwa mambo ya ndani ya nchi.

“NEC imeshazipata asasi za kiraia 245 zitakazokuwa zikitoa elimu ya uchaguzi kwa wananchi wakati wa kipindi hiki kuelekea uchaguzi mkuu na nyingine 97 zitashiriki kama waangalizi wa uchaguzi huo, hivyo zifike mapema ofisi za NEC ili taratibu nyingine ziendelee,” alisema Dk Charles

. Oktoba mwaka huu utafanyika Uchaguzi Mkuu wa Madiwani, Wabunge na Rais ambapo tayari hadi sasa uchukuaji wa fomu za kuwania urais zimeshatolewa na utaratibu wa kuzirejesha umeshaanza.

MBUNGE wa Mbeya mjini Dk Tulia ...

foto
Mwandishi: Mwandishi Wetu

Post your comments

Tangazo

CRDB

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi