loader
Dstv Habarileo  Mobile
Picha

Jaji Nsekela avitaka vyama vya siasa kuzingatia uadilifu

KAMISHNA wa Maadili, Ofi si ya Rais, Sekretarieti ya Maadili ya Viongozi wa Umma, Jaji mstaafu Harold Nsekela ametoa angalizo kwa vyama vya siasa juu ya upitishaji wagombea kwa kuvitaka vizingatie uadilifu wa wahusika.

Akiwasilisha mada katika kikao kazi kati ya vyama vya siasa 19 vyenye usajili wa kudumu na Ofisi ya Msajili wa Vyama vya Siasa, Jaji Nsekela aliwaambia viongozi wakuu wa vyama hivyo kwamba katika kupitisha wagombea wa urais, ubunge na udiwani, sifa ya uadilifu ndiyo iwe kigezo muhimu.

Jaji Nsekela ambaye pia aliwataka viongozi wa vyama kuwa na hofu ya Mungu, alisema, “mkifanya makosa katika hatua ya uteuzi, nchi itegemee kupata viongozi wabovu wasio na maadili. Rushwa ni kichocheo cha kupata viongozi wabovu wasio na maadili.”

Kikao hicho kilichohusu mwenyekiti wa taifa, katibu mkuu na mwanachama anayehusika na masuala ya sheria, alisema wakati wa uchaguzi ndiyo wa kuchora ramani ya aina ya uongozi mpya wa taifa unaohitajika.

Akizungumzia vitendo vya uvunjifu wa maadili katika uchaguzi, Jaji Nsekela alisema kiongozi mwadilifu anapatikana kutokana na utaratibu adilifu na ambao unaaminika. Kwa mujibu wa kamishna huyo wa maadili, kiongozi mwadilifu ni anayetekeleza majukumu kwa uadilifu, anawajibika, ni muwazi, mwaminifu na anazingatia sheria, kanuni na taratibu zilizowekwa.

Alionya juu ya mienendo isiyo ya kimaadili wakati wa uchaguzi ikiwamo kutoa au kukubali kutoa ofisi, mahali au ajira kwa mpiga kura ili kumshawishi kupiga au kuacha kupiga kura. Vitendo vingine ni ukarimu usiokubalika (takrima), kutoa ardhi au kuahidi kutoa fedha au kitu chochote cha thamani ili kushawishi wapiga kura kupiga au kuacha kupiga kura.

Akizungumza na gazeti hili, Naibu Msajili wa Vyama vya Siasa, Mohamed Ali Ahmed alisisitiza umuhimu wa kuwa na vyama vinavyojiendesha kitaasisi.

“Ili kushika dola lazima tuwe na viongozi wanaojielewa na wanaozingatia sheria na taratibu za nchi...kiongozi lazima ajielewe na awe na maadili kama mnavyoona viongozi wa kitaifa wanavyotumia maadili yao kuongoza nchi,” alisema.

Akifungua kikao hicho juzi, Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge, Kazi, Ajira, Vijana na Watu wenye Ulemavu), Jenista Mhagama alivitaka vyama vya siasa kujitathimini juu ya suala zima la maadili ikiwa ni pamoja na kuhakikisha vinashindana kwa hoja badala ya matusi, kejeli na ngumi.

MBUNGE wa Mbeya mjini Dk Tulia ...

foto
Mwandishi: Stella Nyemenohi

Post your comments

Tangazo

CRDB

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi