loader
Dstv Habarileo  Mobile
Picha

Madereva watakaosababisha ajali Wizara ya Elimu kukiona

WIZARA ya Elimu, Sayansi na Teknolojia imewaonya madereva wa wizara hiyo kuwa atakayethubutu kufanya uzembe na kusababisha ajali atachukuliwa kama mhujumu uchumi kutokana na kuitia hasara serikali.

Naibu Katibu Mkuu wa wizara hiyo, Profesa James Mdoe alitoa onyo hilo wakati akifungua mafunzo ya siku tano kwa madereva wa wizara hiyo yakiwahusisha pia na kada ya maofisa waandishi wa taarifa za viongozi na mihutsari kutoka vyuo vya walimu pamoja na vya maendeleo ya wananchi.

Mafunzo hayo yameendaliwa na wizara hiyo kwa kushirikiana na Taasisi ya Uhasibu Tanzania (TIA) na kwa madereva hao ni utekelezaji wa mikakati ya kudhibiti ajali za barabarani zinazochangiwa na baadhi ya madereva wa serikali na kusababisha vifo na majeruhi kwa viongozi na watumishi wa umma.

Profesa Mdoe alisema tathimini iliyofanywa na viongozi wanaowasimamia madereva wa wizara hiyo imebaini baadhi yao wana upungufu mengi hivyo mafunzo hayo maalumu ni muhimu kwa kada hiyo.

Alisema matukio ya ajali za mara kwa mara barabarani zinazochangiwa na madereva wakiwemo wa magari ya serikali ambazo husababisha vifo, majeruhi na uharibifu wa magari yaliyonunuliwa kwa gharama kubwa.

Aliongeza: “Gari unayopewa ni ofisi, gari limenunuliwa kwa gharama kubwa shilingi milioni 200 likiwa jipya baada ya wiki mbili unaligonga tena kwa uzembe, na pia umebeba watu na umepoteza uhai hao...wewe ni sawa na mhujumu uchumi,” alisema Profesa Mdoe.

Kwa mujibu wake, baadhi ya madereva hawazingatii alama za barabarani, kushindwa kuwa na udereva wa kujihami, kukipita chombo kingine cha moto mahali pasipohitajika, wizi wa mafuta na vipuri kwa kushirikiana na mafundi gereji, ulevi na kutoa siri za viongozi wanaowaendesha, kinyume cha sheria za utumishi wa umma.

Maofisa uandishi wa taarifa za viongozi na mihutasari kutoka vyuo vya walimu na vya maendeleo ya wananchi, aliwataka wawe makini na matumizi ya lugha na kujua lugha ya kimandishi ya mawasiliano ya kiserikali.

Mratibu wa mafunzo hayo na Mkufunzi Mkuu kutoka TIA, Dk Hassanal Mwakyoma alisema mafunzo hayo yana lengo la kutatua changamoto mbali mbali zikiwemo vyanzo vya ajali zinazotokea kwa magari ya serikali.

Mkurugenzi wa Rasilimaliwatu na Utawala wa Wizara ya Elimu, Moshi Kabangwe aliupongeza uongozi wa wizara hiyo kuwezesha kwa mafunzo hayo ambayo yanashirikisha madereva 101 na watumishi wengine 30.

Rais John Magufuli amemteua Dk Philemon Sengati kuwa Mkuu wa ...

foto
Mwandishi: John Nditi, Morogoro

Weka maoni yako

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi