loader
Dstv Habarileo  Mobile
Picha

45 mbaroni kwa uhalifu

POLISI mkoani Geita imewanasa watuhumiwa 45 na kuwafungulia mashtaka ambapo kati yao, wamekamatwa wakijaribu kubadilisha noti za dola bandia 2,100, wauza dawa ya kulevya, gongo na wapiga ramli chonganishi.

Akithibitisha uwepo wa matukio na hatua hiyo kwa waandishi wa habari jana ofisini kwake mjini hapa, Kamanda wa Polisi wa Mkoa, Mtatiro Kitinkwi alisema watuhumiwa wamekamatwa kwa nyakati tofauti katika msako maalumu.

Kamanda Kitinkwi alisema miongoni mwa waliokamatwa ni waganga wa kienyeji 10 wanaotuhumiwa kupiga ramli chonganishi wakiwa na vifaa vya kupigia ramli hasa katika wakati huu wa kuelekea Uchaguzi Mkuu, ambao amesema baadhi ya viongozi wa kisiasa hujaribu kuwakingia kifua kwa madai ya kuwa wapiga kura wao.

Alisema watuhumiwa 15 kati yao 13 wamekamatwa na dawa za kulevya aina ya bangi wakiwa na kilogramu 37 na gramu 21 na wengine wawili wakiwa na mafungu 27 ya mirungi, na watuhumiwa 10 wamekamatwa wakiwa na lita 1,232 ya pombe haramu ya gongo.

Alisema watuhumiwa wawili bila kuwataja majina yao, wanashikiliwa kwa tuhuma za kupatikana na noti za dola bandia 2,100 wakijaribu kuzibadilisha katika benki katika Mamlaka ya Mji Mdogo wa Katoro wilayani Geita.

Mbali na na kukamatwa kwa tuhuma hizo, pia amebainisha kuwa watuhumiwa wengine wanne wamekamatwa na kufunguliwa mashtaka ya kupatikana na mali za wizi zikiwemo samani za ndani, televisheni, pikipiki na wengine 10 wamefunguliwa mashitaka saba ya kupatikana na mitambo ya kuchemshia pombe haramu ya gongo. Alisema watuhumiwa sita wamefunguliwa mashtaka ya kupatikana na vifaa vya kupigia ramli chonganishi zikiwamo nyara za serikali.

Rais John Magufuli amemteua Dk Philemon Sengati kuwa Mkuu wa ...

foto
Mwandishi: Mwandishi Wetu, Geita

Weka maoni yako

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi