loader
Dstv Habarileo  Mobile
Picha

Jokate ataka vijana kuchangamkia fursa

MKUU wa Wilaya ya Kisarawe mkoani Pwani, Jokate Mwegelo amewataka vijana wilayani humo kuchangamkia fursa zilizopo huku akiahidi kuwa wilaya hiyo itasonga mbele kimaendeleo.

Amesema hakuna sababu ya vijana kuendelea kubaki nyuma wakati fursa zipo hivyo wahakikishe kila wanachokiona wilayani humo ni fursa, na ni wajibu wao sasa kuchangamkia fursa hizo.

Jokate aliyasema hayo wilayani humo jana wakati akifungua mafunzo kwa vijana 52 kutoka kata mbali mbali ndani ya Kisarawe watakaokuwa wanaongoza watalii wilayani humo na kuratibiwa na Chuo cha Taifa cha Utalii.

“Wilaya ya Kisarawe ina fursa kubwa ya utalii kwani ina vivutio vingi na ukizingatia Mamlaka ya Hifadhi ya Taifa imepandisha hadhi Msitu wa Pugu pamoja na Kazimzumbwi. Na pia kuna mapango mengi ya utalii hivyo zote hizo ni fursa,” alisema DC Jokate.

Aliongeza kuwa Kisarawe katika eneo la utalii imekuwa ni chachu ya kuongeza mapato ya Halmashauri ya Wilaya hiyo ambayo miaka kadhaa ilikuwa inakusanya Sh bilioni moja, lakini sasa wanakusanya Sh bilioni 2.7.

"Pumzika kwa amani Profesa ...

foto
Mwandishi: Mwandishi Wetu, Kisarawe

Post your comments

Tangazo

CRDB

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi