loader
Dstv Habarileo  Mobile
Ummy ataka NHIF kutatua malalamiko ya dawa, vipimo

Ummy ataka NHIF kutatua malalamiko ya dawa, vipimo

MFUKO wa Taifa wa Bima ya Afya (NHIF) umetakiwa kutatua malalamiko ya upatikanaji wa baadhi ya dawa na vipimo kwa wananchi wenye bima ya afya.

Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Ummy Mwalimu alisema hayo jana jijini Dar es Salaam wakati wa kikao na menejimenti ya mfuko huo katika ofisi ndogo za wizara.

“Kumekuwepo na malalamiko ya upatikanaji wa baadhi ya dawa na vipimo kwa watu wenye kadi za bima pia ucheleweshaji wa malipo ya watoa huduma za afya,” alisema Ummy.

Aidha, ameutaka mfuko huo kuendelea kutoa elimu kwa wananchi kuhusu umuhimu wa kujiunga na mfuko huo pamoja na mafao, yanayotolewa katika vifurushi vya bima ya afya.

“Tatueni malalamiko yote kwa wakati ili wananchi wafurahie vifurushi vyote watakavyojiunga navyo,” alisisitiza.

Kikao hicho pia kiliangalia mwenendo wa utoaji wa huduma za bima za afya zinazotolewa na mfuko huo. Kikao hicho kilihudhuriwa na Mku- rugenzi Mkuu wa NHIF, Be- nard Konga, Mkurugenzi wa Tiba katika Wizara ya Afya, Dk Grace Magembe, na Mfamasia Mkuu wa Serikali, Daudi Msasi.

https://apps.tsn.go.tz/public/uploads/a4450dae594f1781fd69188c75fbcf21.jpg

NAIBU Waziri wa Mawasiliano na Teknolojia ya ...

foto
Mwandishi: Mwandishi Wetu

Post your comments

Tangazo

CRDB

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi