loader
Dstv Habarileo  Mobile
Picha

Mndeme aipongeza Ruwasa ujenzi tangi la maji kijijini

MKUU wa Mkoa wa Ruvuma, Christina Mndeme, ameupongeza Wakala wa Maji Vijijini (Ruwasa) wilaya ya Tunduru, kwa kutekeleza vyema mradi wa ujenzi wa tangi la maji katika kijiji cha Milonde, wilayani humo.

Mradi huo wa tangi la kuhifadhia maji ulianza kujengwa Aprili, mwaka huu kwa gharama ya zaidi ya shilingi milioni 215. Hata hivyo, kutokana na matumizi na usimamizi mzuri wa Ruwasa, fedha zilizotumika kujenga mradi huo ni Sh 44,571,372.25 na kubaki Sh 170,940,884.88.

Mkuu huyo wa mkoa alitoa pongezi hizo jana alipotembelea mradi wa maji wa Milonde, ambao utakapokamilika utahudumia wananchi 3,600 wa vijiji vinne vya kata ya Matemanga.

“Nimefurahishwa namna Ruwasa Tunduru ilivyotumia vizuri fedha za miradi ya maji ilizopewa na serikali kuu za ukarabati na ujenzi wa miradi hii ikilinganishwa na miradi inayotekelezwa katika wilaya nyingine za mkoa huu,” alisema.

Mndeme alisema mradi huo ni kati ya miradi bora ya maji inayojengwa na Ruwasa katika mkoa huo, kwani licha ya fedha zilizotumika kuwa kidogo, umekamilika kwa asilimia 90.

“Hapa lazima niwe mkweli, nimevutiwa sana na mradi huu wa maji wa Milonde, kwani licha ya ubora wake, lakini gharama zilizotumika ni kidogo. Nakupongeza sana Meneja wa Ruwasa wa Wilaya ya Tunduru na Mkurugenzi wa Ruwasa Mkoa wa Ruvuma kwa kusimamia vizuri mradi huu, nawaomba hizo fedha zilizobaki zipelekeni zikafanye kazi katika maeneo mengine yaliyobaki,” alisema.

Alisema mradi wa maji Milonde umetokana na maombi ya wananchi kwa Rais John Magufuli alipopita katika kijiji hicho mwaka jana na kumweleza juu ya kero ya muda mrefu ya maji safi na salama na kuwaagiza viongozi wa mkoa wa Ruvuma kushughulikia kero hiyo haraka.

Meneja wa Ruwasa Tunduru, Primy Damas, alisema mradi huo unahusisha pia upanuzi wa mradi wa maji Matemanga na umegharamiwa na serikali kuu kupitia wizara ya maji na kutekelezwa na wakala huo. Alisema ujenzi wa miundombinu ya usambazaji maji ya mradi huo unatarajiwa kukamilika mwezi huu.

SIKU zinahesabika ndani ...

foto
Mwandishi: Muhidin Amri, Tunduru

Post your comments

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi