loader
Dstv Habarileo  Mobile
Picha

NFRA yapangiwa kununua tani 50,000 za mahindi

WAKALA wa Hifadhi ya Taifa ya Chakula (NFRA) Kanda ya Sumbawanga mkoa wa Rukwa imepangiwa kununua tani 50,000 za mahindi katika msimu wa ununuzi unaotarajiwa kuanza katikati ya Julai mwaka huu.

Hayo yameelezwa na Kaimu Meneja NFRA Kanda ya Sumbawanga, Mara Range katika mahojiano maalumu na gazeti hili mjini hapa. Alisema kwa sasa wakala huo umeanza kununua tani 5,000 za mahindi ambayo ni ya msimu uliopita wa mavuno.

Alisema mahindi hayo yameanza kununuliwa tangu Mei, 25 mwaka huu ambapo kwa mjini kilo moja inanunuliwa kwa bei ya reja reja ya Sh 550 huku vijijini bei ikiwa ni Sh 500.

‘Bei hii inatoa ahueni kwa wakulima kwa sababu kwa sasa vijijini kilo moja ya mahindi inanunuliwa kwa bei ya Sh 300 ambapo gunia moja la mahindi lenye uzito wa kilo 100 ni Sh 30,000 huku mjini likiuzwa kwa Sh 40,000.

Hakuna masharti watu wote wanaruhusiwa kuuza mahindi yao NFRA yaani hakuna masharti kwa vikundi vya wakulima wala watu binafsi ...isipokuwa yawe meupe yawe na unyevunyevu usiozidi asilimia 13,” alifafanua.

Aliongeza kuwa mpaka sasa wakala huo umeshanunua kilo 1,657 za mahindi katika vituo vya Mazwi mjini Sumbawanga, Laela na Mtowisa katika Halmashauri ya Wilaya ya Sumbawanga mkoani Rukwa. Pia katika vituo vya Kibaoni na Milumba vilivyopo mkoani Katavi.

SIKU zinahesabika ndani ...

foto
Mwandishi: Peti Siyame, Sumbawanga

Post your comments

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi