loader
Dstv Habarileo  Mobile
Picha

Bakwata yataka uchaguzi wa amani 2020

BARAZA la Waislamu Tanzania (BAKWATA) Mkoa wa Pwani limewataka wajumbe kuhakikisha Uchaguzi Mkuu unafanyika kwa amani na utulivu na kupata viongozi bora wenye mshikamano kwa ustawi wa wananchi.

Hayo yamesemwa mjini Kibaha na Kaimu Shehe wa Mkoa, Hamis Mtupa wakati wa mkutano wa uchaguzi wa baraza la mkoa kuchagua viongozi wake watakaoongoza kwa miaka mitano ijayo.

Mtupa alisema viongozi hao wana jukumu la kumwomba Mungu kujiandaa na Uchaguzi Mkuu ujao kwani huo ni wajibu wao na wana jukumu hilo ili kuhakikisha ustawi wa amani na utulivu katika nchi kwa kutoa elimu kwa waumini na Watanzania kupitia vikao mbali mbali ili wawe na mshikamano na ili wasishawishiwe kuchagua viongozi wale wanaopenda kuingia madarakani kwa lugha za umwagaji damu.

“Tanzania haitakuwa na amani endapo damu itamwagika mna jukumu la kuhakikisha uchaguzi unafanyika kwa utulivu kwa kuwa nanyi mnakuwa sehemu ya amani na utulivu kwa kuwaelekeza wananchi kuchagua viongozi bora waakoleta maendeleo na kuivusha nchi,” alisema Mtupa.

Alisema Watanzania wamwombe Mungu ili awapatie viongozi wenye huruma na kulinda rasilimali za nchi ili zilete maendeleo kwa wananchi kwani viongozi ambao hawana huruma hawataweza kuwatumikia wananchi, bali watakuwa wanajinufaisha wao.

Wamemshukuru Mungu kwa kuiponya Tanzania kwa wananchi wake kutoshambuliwa kwa kiasi kikubwa na Covid-19, ambao haukuathiri kwa kiasi kikubwa kama ilivyo nchi nyingine zikiwemo jirani.

Alisema Mungu ndiye mweza wa yote lakini pia walimpongeza Rais John Magufuli kuivusha nchi katika janga la corona kutokana na msimamo wake kwa kutofunga nyumba za ibada, hivyo kuwawezesha wenye imani kumwomba Mungu na kutaka wauone ugonjwa huo kama magonjwa mengine kwa kuwatoa hofu.

“Katika Covid-19, Rais alikuwa na msimamo uliofanya Tanzania kuheshimika kwani alikataa kuwafungia Watanzania na kuwataka kuchukua tahadhari huku wakiendelea na shughuli zao za kila siku za ujenzi wa Taifa,” alisema Shehe Mtupa.

Aidha, alimpongeza Mufti na Shehe Mkuu wa Tanzania, Abubakary Zubeir kwa mabadiliko makubwa kwa Bakwata kwani imekuwa na hadhi kwa hasa kwa taasisi za Kiislamu kuwa na ushirikiano na taasisi zisizo za Kiislamu kwa kutobaguana na kushirikiana na wengine katika masuala ya kimaendeleo.

Katika uchaguzi huo uliosimamiwa na Rajabu Mruma kutoka Makao Makuu ya Bakwata, Hamis Masasa alichaguliwa kuwa Mwenyekiti wa Halmashauri ya Bakwata Mkoa akipata kura zote 27, wakati Mjumbe wa Halmashauri Taifa, Adam Mwasha alipata kura 14 akimshinda Ally Jandumbo aliyepata kura 12.

Wajumbe wa Baraza la Mashehe Mkoa wa Pwani walikuwa wagombea saba na kupitishwa Amas Mzee, Lafir Hemed, Mustafa Doga, Zuberi Chamgunda, Athuman Mtasha, Nuhu Nkera na Abdala Omary.

Wajumbe wa Halmashauri ya Mkoa walikuwa wagombea saba nao waliopitishwa ni Jamal Mtanga, Mohamed Kiaratu, Ally Mwasingo, Abdala Athuman, Riziki Majala, Sadiq Mlahagwa na Sudi Kihamaya.

Wagombea kutoka vyama vya ...

foto
Mwandishi: John Gagarini, Kibaha

Post your comments

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi