loader
Dstv Habarileo  Mobile
Picha

Rais Burundi aunganisha wizara

BARAZA jipya la mawaziri nchini Burundi, lililoteuliwa na Rais mpya, Evariste Ndayishimiye (pichani), lina mawaziri 15, wanaume 10 na wanawake wa watano.

Baraza hilo lina tofauti ya wizara sita za baraza la zamani la serikali ya hayati Rais Pierre Nkurunziza, lililokuwa na mawaziri 21. Katika baraza jipya, Wizara ya Usalama, Mambo ya Ndani na Maendeleo ya Jamii zimewekwa pamoja na kuwa wizara moja inayoongozwa na Gervais Ndirakobuca. Ndirakobuca ni ofisa wa ngazi ya juu katika Polisi.

Alikuwa mkuu wa idara ya upelelezi katika serikali ya Nkurunziza. Wizara za Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC), Vijana, Michezo na Utamuduni nazo pia zimejumuishwa pamoja na kuwa wizara moja inayoongozwa na aliyekuwa Waziri wa Mambo ya Nje, Ezechiel Nibigira.

Wizara ya Mambo ya Nje sasa inaongozwa na aliyekuwa Balozi wa Burundi katika Umoja wa Mataifa (UN), Albert Shingiro. Wizara ya Ulinzi kwa mara nyingine inaongozwa na raia.

Hii ni mara ya kwanza tangu mwaka wa 1976 kwa Burundi kuongozwa na rais ambaye ni Jenerali wa Jeshi na Waziri Mkuu ambaye ni ofisa wa cheo cha juu katika Jeshi la Polisi, Alain Guillaume Bunyoni.

Mawaziri wa zamani katika serikali ya hayati Nkurunziza ambao wameshikilia nyadhifa zao katika serikali mpya ni wa Fedha, Elimu na Utafiti wa Sayansi, Afya na Kilimo na Ufugaji. Mawaziri wengi wapya ni kutoka chama tawala cha CNDD-FDD.

KIONGOZI wa upinzani, Raila Odinga, amewatahadharisha Wakenya juu ya siasa ...

foto
Mwandishi: BUJUMBURA, Burundi

Post your comments

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi