loader
Dstv Habarileo  Mobile
Picha

JPM ampongeza Rais mpya Malawi

RAIS John Magufuli amempongeza Rais mpya wa Malawi, Dk Lazarus Chakwera kwa kuchaguliwa kuongoza nchi hiyo.

Dk Chakwera alitangazwa na Tume ya Uchaguzi ya Malawi kuwa mshindi wa urais wiki iliyopita ;na Jumapili aliapishwa kuliongoza taifa hilo, baada ya matokeo ya uchaguzi wa awali kutenguliwa.

Rais Magufuli aliandika katika ukurasa wake wa twitter, “Nakupongeza Dk Lazarus Chakwera kwa kuchaguliwa kuwa Rais wa Jamhuri ya Malawi.

“Kwa niaba ya Serikali na Watanzania wote naahidi kuendeleza uhusiano wetu wa kidugu, kirafiki na ujirani mwema hususani katika masuala ya uchumi na ustawi wa jamii. Hongera sana Mheshimiwa rais,” alisema Rais Magufuli kupitia ukurasa wake wa twitter jana.

Dk Chakwera aliyeanza kuteua baraza lake la mawaziri juzi, alishinda uchaguzi wa marudio kwa asilimia 58.57 (59) ya kura zilizopigwa.

Watu waliojitokeza kupiga kura ni milioni 6.8 sawa na asilimia 64.81 ya waliojiandikisha. Mahakama ya Katiba ya Malawi iliamuru uchaguzi urudiwe kutokana na kubaini ukiukwaji wa kikatiba katika uchaguzi wa Mei 2019 uliompa ushindi aliyekuwa Rais Peter Mutharika.

Malawi imekuwa nchi ya pili Kusini mwa Jangwa la Sahara kuwa na uchaguzi wa marudio wa rais, baada ya mahakama kutengua wa awali.

Kenya ilikuwa ya kwanza mwaka 2017. Chakware juzi alianza kutangaza baraza lake la mawaziri lililowakumbuka watu waliomsaidia katika kushinda kesi ya kupinga matokeo akiwamo mgombea mwenza na Makamu wa Rais wa nchi hiyo, Saulos Chilima aliyemteua kuwa Waziri wa Mipango ya Uchumi, Maendeleo na Maboresho ya Sekta Binafsi.

MWITO umetolewa kwa wakulima kwenye mikoa yanayozalisha chakula kwa wingi ...

foto
Mwandishi: Gloria Tesha

Post your comments

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi